HIJAMA NI NINI?

Faida za Kuumika/Chuku/HIJAMA

Kitendo cha kuumika ni sunna ya Mtume Muhammadi ( ﷺ ) na imepokewa mara nyingi sana katika hadith zilizo sahihi. Kuumika ni kitendo kilichohimizwa na kutiliwa mkazo katika mapokezi mengi. Kuumika ni sehemu ya mfumo unaokamilisha Tiba ya kiutume ya Kiislamu.
Kuumika kulikuwa zoezi la kawaida la Mtume Muhammad ( ﷺ ) na Maswahaba zake kwa kutibu maradhi na magonjwa mengi na hata kuukinga mwili na kuboresha afya.

Maana Yake
Hijama au kuumika ni salama, isiyokuwa na madhara na njia isiyogharimu katika kutibu na kuzuia maradhi. Ijapokuwa matumizi ya Wachina katika mfumo huu matibabu yao yameengemezwa katika sehemu chache kama matatizo ya mapafu, mafua, kutibu maradhi ya viungo vya ndani, maumivu ya viungo, nk. Uwezo wa kuumika au hijama na faida zake ni kubwa zaidi kuliko mapungufu au hasara zake.
Neno Hijama linamaanisha ‘kutoa’ kwa Kiarabu. Kwa sasa inatambulika kama njia mbadala ya tiba ya kutibu maradhi mbali mbali na magonjwa mengine katika mwili. 
Matibabu ya kisayansi ya sasa pia yanakubaliana na faida mbali mbali za hijama au kuumika na hata kupendekeza matumizi yake katika maradhi mbali mbali.
Katika taratibu hizi ambazo si za kiupasuaji, sumu au damu chafu hutolewa kutoka katika mwili. Baadhi sehemu za hijama au kuumika katika mwili hutumika Katika sehemu hizo zilizochaguliwa, damu husababishwa kuwa katika sehemu hiyo alafu hunyonywa na kwa kutumia mfumo wa bomba, chupa au chombo kisichokuwa na chochote ndani yake. 

Faida Zake
Kuumika ni mbinu za kale za kutoa damu chafu ambayo ilikuwa ikitumika katika nchi nyingi katika kutibu baadhi ya Maradhi au magonjwa mengine ya mwili. Wakati Wachina wanaonekana kwamba wanaongoza katika matumizi ya mbinu za kutoa damu chafu kwa kutibu maradhi mbali mbali, Waarabu wamerithi kama sunna iliyokokotezwa na Mtume Muhammad ( ﷺ ) .WAzungu nao walikuwa wanafanya hijama au kuumika katika kutibu baadhi ya maradhi. Tofauti iliyopo baina ya Waarabu au Waislamu na wengine katika kuumika au hijama ni kwamba ilifanyika kwa wazi na Waumini walipendezwa nayo sana kama ni sunna ya Mtume Muhammad ( ﷺ ) (bila ya kuuliza chochote) na wengine wanaifanya kama faida ya kimatibabu.

Faida ya kwanza kabisa na inayoongoza ya kuumika au hijama kwa muumin ni faida atakayoipata hapa duniani na kesho akhera, baada ya kufuata sunna iliyokokotezwa ya Mtume Muhammad ( ﷺ ). Si waumini peke yao ila kila mtu anakaribishwa kuchunguza au kupata uzoefu juu ya faida walizotunikiwa waumini kwa kufuata amri za Mwenyezi Mungu na Mtume wake ( ﷺ ) kwa upande mwingine, tunapoaangalia mbinu hizi za kutoa damu chafu kwa mtazamo wa kidunia tunagundua kwamba kuumika au hijama ina faida nyingi sana.

Inafahamika kwamba kuumika au hijama inasaidia kuongeza nguvu katika damu. Inaondoa sumu na uchafu katika damu.Inaharakisha uponyaji wa haraka na watu hupona maradhi haraka baada ya kuumika au hijama. Kuumika au Hijama inafahamika kwa kuzuia maradhi na kwa hiyo inaweza kusadikika kama inaongoza katika ukingaji wa maradhi mengi. Zaidi ya hayo, pia ianfahamika kwamba kuumika au hijama inaweza kuwasaidia wale watu ambao wamekumbwa na uchawi au wamepatwa na Jini.

Kuumika au hijama haina madhara kama itatekelezwa vizuri. Ni vizuri ukafahamu kwamba asilimia 70 ya maradhi au magonjwa yoyotehutokana kushindwa kwa damu kuzunguka vizuri katika mwili. Ziadi ya hilo huwa tuna kuwa wagonjwa au viungo vyetu kushindwa kufanya kazi wakati damu yetu inayozunguka mwilini imeajaa sumu na uchafu mwingine. Bila ya kuondoa sumu katika miili yetu au kutoka kwenye damu, si tu kwamba hatutapona haraaka kutokana na maradhi yanayotusumbua ila pia tunakaribisha maradhi mengine au magonjwa. Kuumika au hijama ndiyo njia sahihi ya kuondoa sumu kutoka mishipa ya damu, na matokeo yake bila ya shaka yatakusababishia kuwa na afya nzuri na mwili unaofanya kazi vizuri. Tusisahau kwamba njia hii nzuri na yenye kusaidia imependekezwa na sunna ya Mtume Muhammad ( ﷺ ) inatusaidia kujikingana maradhi mengi na maambukizi kama shinikizo la damu, magonjwa yanayotokana na mzunguko wa damu, maumivu, ugumba na utasa, kansa nk 

Umuhimu wa Kuumika au Hijama kutokana na muongozo wa Wahyi.
Kuliko kuweka maneno zaidi katika kutaja sifa na ubora wa kuumika, ni vizuri tukaziangalia hadith zifuatazo ambazo zinatosheleza kuelezea faida na umuhimu wa Kuumika au Hijama.
“Kwa kweli kwenye Kuumika au hijama kuna dawa.” – Sahihi Muslim
“kwa kweli, tiba ilyo bora mliyonayo ni kuumika au hijama.” – Sahihi Bukhari
“Kuumika ni njia bora zaidi kwa wanadamu katika kujitibu.” ”.– Sahihi Bukhari na Sahihi Muslim
Umuhimu wa Kuumika katika muongozo wa kiroho unaweza kusisitizwa kwa maneno yafuatayo ambayo aliambiwa Mtume Muhammad ( ﷺ ) katika usiku wa Israa na malaika: “Ewe Muhammad, waamrisha umma wako kuhusu kuumika.” – Sahihi Muslim, Sunan Tirmidh

Mtume Muhammad ( ﷺ ) inasemakana alihumikwa katika kichwa chake kutokana na kuumwa kipandauso (Bukhari), katika kidole chake cha mguu kutokana na kutenguka (Ibn Majah) katika shingo yake (Abu Daud), katika nyonga kutokana na maumivu ya nyonga (Abu Daud) na mabega kwa ajili ya kutoa sumu (Ahmed).

Abdullah ibn Abbas (Mwenyezi Mungu awe radhi nae) amesimulia kwamba Mtume ( ﷺ ) amesema: “sikumpita malaika yoyote katika safari yangu ya usiku isipokuwa aliniambia: kilicho bora ni Kuumika, Ewe Muhammad.” (Sahihi Bukhari, Sunan Ibn Majah)

“Dawa iliyobora ambayo unaweza kujitibia ni kuumika, au ni miongoni mwa dawa bora kabisa au Dawa unaweza kuitumia ni kuumika.”(Sahihi Bukhari:5371) 

“Kuumika ni taratibu iliyo namanufaa zaidi kwa wanadamu kwa ajili ya kujitibu.” (Sahihi Bukharin a Muslim)
#)Pilingu #RUQYA #HIJAMA SIYO #PIRINGU

Abu Huraira (Mwenyezi Mungu awe radhi nae) amesimulia kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ( ﷺ ) amesema:”Kama kungekuwa na kitu bora kinachoweza kutumika kama dawa basi ni kuumika.” *Sunan Abu Dawud, Sunan Ibn Majah)
Gusa maandishi haya ili kutazama video ya Hijama.
©
Sheikh Pilingu 
Ruqya & Hijama Center 
Mbagala Charambe Daressalaam 
+255713494945