HEKIMA YA KULETWA MITUME.

MwenyeziMungu anasema:- "Bila shaka tumempeleka Mtume katika kila umma (awaambie) ya kwamba "Mwabuduni MwenyeziMungu na muepukeni (Iblis) muovu". (An - Nahl -36)

MAISHA YA BARZAKH (BAADA YA KUFA)

MwenyeziMungu anasema: "Hapana! Hakika hili ni neno tu analolisema yeye (aliye mwovu anapofikiwa na mauti) na mbele yao kuna maisha ya baada ya kufa (ya taabu kwa wabaya na ya raha kwa wazuri) mpaka siku watakapofufuliwa!". (Al - Muminun - 100)

VITISHO VYA SIKU YA KIAMA

Na katika kauli Yake:- "(Wakumbusheni) Litakapotokea tokeo (hilo la Kiama). Ambalo kutokea kwake si uwongo. Lifedheheshalo (wabaya). Litukuzalo (wazuri). Ardhi itakapotetemeshwa mtetemeko mkubwa. Na milima itakaposagwa sagwa. Iwe mavumbi yanayopeperushwa". (Al - Waqiah - 1 - 6)

KUMTII MWENYEZIMUNGU NA KUMTII MTUME WAKE(SAW)

MwenyeziMungu anasema:- "Na wenye kumtii MwenyeziMungu na Mtume, basi hao watakuwa pamoja na wale aliowaneemesha MwenyeziMungu; Manabii na Masidiki na Mashahidi na Masalih (watu wema). Na uzuri ulioje (kwa mtu) watu hao kuwa rafiki (zake).” (An - Nisaa -69)

KUTOKA KATIKA DINI -"KUR-TADI"

MwenyeziMungu anasema:- "Wala hawataacha kupigana nanyi, mpaka wakutoeni katika dini yenu, kama wakiweza. Na watakaotoka dini yao katika nyinyi, kisha wakafa hali ya kuwa makafiri, basi hao ndio ambao amali zao zimeharibika katika dunia na akhera. Nao ndio watu wa Motoni. Humo watakaa milele." (Al - Baqarah -217).

DAWA YA NGOZI. (Mba, upele, Chunusi, Fangasi, Miwasho, Malengelenge, Mapunye, Utangotango n.k.


1. Mafuta ya habasoda changanya na mafuta ya waridi na ngano nyukundu- vyote ujazo sawa ila ngano izidi kisha upake kutwa X2 au soma 1:1 au 57:4

KUUNGUA MOTO
2. Ngozi iliyoteketea kwa moto paka asali iliyo changanywa na ute wa yai.

FANGASI
3. Kibiritu azraqu na aswfaru na maziwa ya cowball na mafuta paka kutwa X2

4.Changanya sufa na asali na unywe kijiko 1X3

5.Soma dawa namba 9

6.Changanya mafuta ya H.soda na mafuta ya wardi na ngano nyekundu. Vyote ujazo sawa ila ngano iweX2 paka kutwa X2

NGOZI ILIYOTEKETEA KWA MOTO

7.Changanya asali na ute wa yai kasha paka.

8.Changanya maziwa ya Cowbell na Kibritu aswataru na mafuta yoyote. Paka X2

FANGASI BAINA YA MAPAJA
9.Paka mafuta ya H.saoda kabla ya kulala. Siku 7

10.Majani ya Mrehani sugua kichwani pia hutunza nywele kung’oka na na kuzifanya ziwe nyeusi

11.Changanya mafuta ya Habasoda na mafuta ya Zaituni paka pale palipo athirika

12.Changanya kwa ujazo sawa mafuta ya Habasoda Mafuta ya Mdarasini, mafuta ya Ndimu na Mafuta ya Kitunguu Thaumu.
Chemsha kisha paka kutwa x2.