HEKIMA YA KULETWA MITUME.

MwenyeziMungu anasema:- "Bila shaka tumempeleka Mtume katika kila umma (awaambie) ya kwamba "Mwabuduni MwenyeziMungu na muepukeni (Iblis) muovu". (An - Nahl -36)

MAISHA YA BARZAKH (BAADA YA KUFA)

MwenyeziMungu anasema: "Hapana! Hakika hili ni neno tu analolisema yeye (aliye mwovu anapofikiwa na mauti) na mbele yao kuna maisha ya baada ya kufa (ya taabu kwa wabaya na ya raha kwa wazuri) mpaka siku watakapofufuliwa!". (Al - Muminun - 100)

VITISHO VYA SIKU YA KIAMA

Na katika kauli Yake:- "(Wakumbusheni) Litakapotokea tokeo (hilo la Kiama). Ambalo kutokea kwake si uwongo. Lifedheheshalo (wabaya). Litukuzalo (wazuri). Ardhi itakapotetemeshwa mtetemeko mkubwa. Na milima itakaposagwa sagwa. Iwe mavumbi yanayopeperushwa". (Al - Waqiah - 1 - 6)

KUMTII MWENYEZIMUNGU NA KUMTII MTUME WAKE(SAW)

MwenyeziMungu anasema:- "Na wenye kumtii MwenyeziMungu na Mtume, basi hao watakuwa pamoja na wale aliowaneemesha MwenyeziMungu; Manabii na Masidiki na Mashahidi na Masalih (watu wema). Na uzuri ulioje (kwa mtu) watu hao kuwa rafiki (zake).” (An - Nisaa -69)

KUTOKA KATIKA DINI -"KUR-TADI"

MwenyeziMungu anasema:- "Wala hawataacha kupigana nanyi, mpaka wakutoeni katika dini yenu, kama wakiweza. Na watakaotoka dini yao katika nyinyi, kisha wakafa hali ya kuwa makafiri, basi hao ndio ambao amali zao zimeharibika katika dunia na akhera. Nao ndio watu wa Motoni. Humo watakaa milele." (Al - Baqarah -217).

UTAMJUAJE MTU ALIYEATHIRIKA NA UCHAWI AU MAJINI?.

1.  Kuumwa kichwa upande mmoja,meno,mgongo,kiuno na kubanwa kifua. 2.  Kuumwa tumbo chini ya kitovu hii ni kwa akinamama. 3.  Moyo kwenda mbio na kushtuka bila asbabu. 4.  Kushika moto mwili hasa miguu pmj na ganzi na maumivu makali. 5.  Kizunguzungu mara kwa mara. 6.  Kuumwa tumbo sana kwa akinamama wakati wa period pmj na kutoa damu nyingi au chache sana. 7.  Kupata maumivu makali wakati wa jimai kwa akinamama na kukosa hamu ya tendo hilo au kulichukia kabithaaaa. 8.  Kutembelewa na vitu mwilini. 9. ...