UGONJWA WA PID.

UGONJWA WA PID (Pelvic Inflammatory Disease) au Maambukizi Katika Mfumo wa Uzazi wa Mwanamke. Mara nyingi dactari wengi uchanganya wakafikiri ni UTI

Magonjwa ya zinaa ndio sababu kuu ya wanawake kupata maambukizi katika mfumo wa uzazi yani (PID). Mwanamke 1 kati ya wanawake 8 walipota PID katika wakati wowote ndani ya maisha yao hupata tabu kushika mimba.

(PID) NI NINI?
PID ni maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mara nyingi husababishwa na magonjwa ya zinaa kama gonorrhea na chlamydia ila kuna aina ya maambukizi mengine mbali na magonjwa ya zinaa yanaweza kusababisha maambukizi ya PID.

JE! MWANAMKE HUAMBUKIZWAJE PID?
Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa PID. Njia hizo ni pamoja na:

- Kama una ugonjwa wa zinaa na haijatibiwa
- Kufanya ngono zembe isiyo salama (yani kulala na wanaume tafauti tafauti)
- Kuwa na mpenzi ambaye ana wanawake wengi nnje
- Kama umekuwepo na historia ya PID hapo nyuma
- Maambukizi ya njia ya uzazi hasa kipindi mara baada ya kujifungua (au postpartum period)
- Maambukizi ya njia ya uzazi mara baada ya kutoa mimba kwa njia zisizo salama (post abortion) au mara baada ya mimba kutoka (miscarriage)
- Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi (IUCD) kama njia mojawapo ya uzazi wa mpango
- Kuambukizwa kupitia damu iliyo na vimelea vya PID
- Kutumia (Vaginal Dauche)

UTAJUAJE UTAJUAJE KAMA UNA(PID)?
Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID. Miongoni mwa dalili hizi ni:

- Mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu
- Kupata maumivu ya mgongo
- Mwanamke kupata utoko mchafu sehemu za siri. Utoko huu huambatana na harufu mbaya.
- Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
- Kupata maumivu au kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa
- Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi
- Kupata homa
- Kupata damu innje ya siku zako zako za-kawaida kupata damu ya hedhi
- Wakati fulani kuhisi kichefuchefu kama mwanamke mja mzito na kutapika

VIPIMO VYA PID
Hakuna vipimo maalum kudhibitisha mwanamke ameathirika ila Dactari hujua mwanamke ameathirika baada ya kuchukua historia ya muhusika na kufanya vipimo vingine kama:

- Kuchunguza mkojo ili kufahamu kama mgonjwa ana mimba. Kipimo hiki ni muhimu hasa kwa mwanamke aliye katika umri wa kuzaa au mwenye uwezo wa kubeba mimba
- Uchunguzi wa mkojo kwenye darubini ili kutambua aina za vimelea vinavyomletea mgonjwa uambukizi. Aidha mkojo huweza kuoteshwa katika maabara kwa ajili ya kutambua aina nyingine za vimelea viletavyo uambukizi huo.
- Kupima damu kwa ajili ya kuchunguza jinsi aina mbalimbali za chembe za damu zilivyoathiriwa na uambukizi huo au kama kuna mwingiliano na magonjwa mengine yaliyojificha. Kipimo hiki kwa kitaalamu huitwa (Full Blood Picture).
- Kuchukua utando unaozunguka shingo ya uzazi na kuuotesha kwa ajili ya utambuzi wa aina za vimelea viletavyo maambukizi hayo. Kipimo hiki huitwa (Cervical culture)
- Aidha ni muhimu pia kufanya vipimo vingine kwa ajili ya utambuzi wa magonjwa yaambukizwayo kwa njia ya kujamiiana, kama vile virusi vya ukimwi na kisonono.
- Mgonjwa pia anaweza kufanyiwa ultrasound ya nyonga ili kuangalia kama kuna athari yeyote katika mfumo wake wa uzazi.

JE PID INAWEZA KUTIBIWA?
Jibu ni ndio kama itagunduliwa mapema inaweza kutibiwa na ikaisha, ila ieleweke kama tayari ilikuwa imeharibu njia za uzazi uharibifu ule haiwezi kurekebishwa. Kila mara ukichelewesha kutibu PID ndivyo itaharibu mfumo wako wote wa uzazi sasa ni muhimu ukiona mojawapo wa dalili nilizozitaja utembelee daktari ili upate tiba. Hata kama utatibiwa na zile dalili zikapotea hakikisha kila mara unashauriana na daktari wako na ukipata mume mwingine ni muhimu umueleze ili mpate matibabu msi-ambukizane mara kwa mara. Ijulikane kama ulikuwa na PID awali inaweza kurudi mara kwa mara.

MATIBABU
Mara mgonjwa anapogunduliwa kuwa ameathiriwa na ugonjwa huu, dawa za jamii ya antibayotiki huweza kutumika kwa ajili ya kuua vimelea vya ugonjwa.

Au
Kwa Dawa za Asili
Chukuwa Hulba na Manjano changanya pamoja. Kisha chota kikombe 1 Kunywa m
Ieleweke pia mara nyingi ugonjwa hujirudia mara kwa mara kama mwanamke atapewa tiba na mume asitibiwe. Na kama maambukizi imekuwa sugu inabidi muathiriwa amueleze daktari ili apate kutumia anti-biotics kwa mda mrefu kuliko kawaida. Lakini muhimu sana mwanaume apewe dawa wakati mwanamke anatibiwa. Ikiwa mwanamke peke yake atapata tiba pindi atakapo lala na mwanaume yule yule maambukizi yatarejelea.

MADHARA YAKUTO-FWATA MATIBABU
- Maumivu ya mfuko wa uzazi wakudumu
- Utapata ugumu wa kushika mimba
- Ectopic pregnancy (mtoto kuwa innje ya mfuko wa uzazi)
- Kuziba kwa njia ya uzazi

JINSI YA KUZUIA MAAMBUKIZI
Kuna njia kadhaa za kuzuia maambukizi katika mfumo wa uzazi. Njia hizi ni pamoja na:

- Njia hakiki ya kujizuia na maambukizi haya ni kuwacha ngono zembe na kufanya ngono salama ndani ya ndoa halali kwani zina ni haramu, kama utakuwa mwenye kutaka dhambi basi tumia kondomu ili usiwaambukize watu wengine
- Kuwahi kuwaona wataalamu wa afya mara dalili za ugonjwa huu zinapoanza kujitokeza au pindi tu unapogundua kuwa mwenzi wako ana dalili za magonjwa ya zinaa au anatembea na wanawake wengine
- Kufanya vipimo mara kwa mara hasa vya mfumo wa uzazi, pamoja na vipimo vya maambukizi ya magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya ngono (STI) khususan ugonjwa wa chlamydia ufanyie vipimo kila mwaka mara 1
- Kutofanya ngono mara baada ya kujifungua, mimba kutoka ili kuhakikisha njia ya shingo ya uzazi imefunga vema.

Sheikh Pilingu Hijama & Ruqya Center
0713494945