FAHAMU UGONJWA WA KANSA DALILI NA TIBA YAKE.


KANSA au kwa jina jingine, Saratani, ni kundi la magonjwa yanayosababishwa na mgawanyiko usio sawa na usiodhibitika wa seli na kuunda uvimbe unaovamia na kuzidhuru tishu za mwilini. Kansa isiyotibiwa, inaweza kuwa ugonjwa unaoshambulia tishu nyingine mwilini na kusababisha kifo.

Kwa kawaida, kansa huusababishia mwili madhara pale inapoharibu seli na kuzifanya zigawanyike bila kudhibitika na kuwa uvimbe wa tishu unaojulikana kama tumor, isipokuwa katika kansa ya damu ambapo kansa huzuia utendaji wa kawaida wa damu kwa kuzifanya seli ziwe na mgawanyiko usio wa kawaida katika damu.

Historia ya Kansa

Asili ya neno kansa linatokana na daktari bingwa wa Ugiriki aliyeishi kati ya miaka 460 na 370 (K.K) anayejulikana kwa jina la Hippocrates. Hippocrates alitumia maneno 'Carcinos' na 'Carcinoma' kuelezea uvimbe unaotengeneza mchubuko (Carcinos) kwa upande mmoja, na uvimbe usiotengeneza mchubuko (Carcinoma) kwa upande wa pili.

Maneno haya ya Kigiriki, yana maana ya mdudu kaa. Hii ni kwa sababu ugonjwa ho wa kansa ulipogunduliwa kwa mara ya kwanza ulifananishwa na mdudu kaa kwa kuwa ulikuwa ikisambaa kila upande kama miguu ya mdudu kaa.

Kati ya miaka 25 na 50 (K.K), Daktari Bingwa mwenye asili ya Roma, aliyejulikana kwa jina la Celsus alitafsiri maneno hayo kwa neno la Kilatini, kwa kuita 'Cancer' likiwa na maana ya mdudu kaa. Miaka kati ya 130 na 200 (B.K), Daktari Bingwa mwingine kutoka Ugiriki, alitumia neno 'Oncos' likiwa na maana ya ‘kuvimba’ kuelezea uvimbe tofauti usiosambaa.

Hata hivyo, maneno ya Hippocrates na Celsus, ya 'Carcinos' na 'Cancer' yenye maana ya mdudu kaa ambayo bado yanatumika hadi leo kuelezea uvimbe unaosambaa, neno la Galen 'Oncos' linatumika tu kama sehemu ya somo linalohusu kansa (Oncology) au madaktari wa kansa (Oncologist
[8/29, 21:16] ‪+254 722 920271‬: Ni nini chanzo cha ugonjwa wa kansa?

Mwili wa binadamu umeundwa kwa trilioni za seli ambazo hukua, kugawanyika na kufa kwa mpangilio maalumu. Mwenendo ulioratibiwa vyema unasimamiwa na vinasaba (DNA) vilivyo ndani ya seli. Vinasaba hivyo, vinapatikana katika kila seli, na huongoza matendo yote yanayofanywa na seli. Katika seli ya kawaida, wakati vinasaba vinapoharibika, seli hukarabati au seli hufa.

Lakini katika seli za kansa, kinasaba kilichoharibika huwa hakiwezi kukarabatiwa na seli haifi kama inavyotakiwa, badala yake huendelea kutengeneza seli nyingine ambazo hazitakiwi na mwili na hivyo seli hizo mpya zote huwa na kinasaba kisichokuwa cha kawaida tofauti na seli salama.

Watu huweza kurithi kinasaba kisichokuwa cha kawaida, ingawa mara nyingi uharibifu wa kinasaba husababishwa na makosa yanayotokea wakati seli ya kawaida inapotengenezwa au kutokana na sababu za kimazingira. Ingawa inajulikana wazi kwamba kuna baadhi ya vitu vinavyoweza kuharibu kinasaba na kusababisha kansa, kama vile kemikali, uvutaji sigara, kuchomwa na jua na kadhalika, lakini bado hakuna uhakika wa moja kwa moja kuhusiana na kinachosababisha kansa.

Wakati mtu anapokuwa mtoto mdogo au bado akiwa ndani ya tumbo la mama, seli hujigawanya kwa haraka ili kumfanya akuwe.
Baada ya mtu kukua, seli nyingi hugawanyika kwa ajili ya kuchukua nafasi ya zile zilizozeeka na kufa au kwa ajili ya kukarabati majeraha.

Kansa huanza wakati seli katika sehemu mojawapo ya mwili zinapoanza kukua bila kudhibitiwa. Ukuaji wa seli za kansa hutofautiana na ukuaji wa kawaida wa seli za mwili, na badala ya kufa pale zinapozeeka, zenyewe huendelea kukua na kuzaa seli nyingine mpya zisizokuwa za kawaida.

Seli za kansa pia hushambulia kwa kuingia ndani ya tishu nyigine jambo ambalo halishuhudiwi katika seli za kawaida. Kwa kawaida seli za kansa husambaa katika sehemu nyingine za mwili ambako huko nako, huanza kukua na kuunda uvimbe (tumor) mpya na baada ya muda kupita uvimbe huo huchukua nafasi ya tishu mpya.

Kwa hiyo, kukua kusikodhibitiwa na kusiko kwa kawaida kwa seli, na tabia ya seli hizo kuzishambulia tishu nyingine, ndiko hasa husababisha seli za kansa.

Sifa za ugonjwa wa kansa

Si kila uvimbe ni kansa, bali kuna uvimbe ambao si kansa, ambao kitaalam huitwa 'Benign Tumors', kama vile Tezi dume (Benign Prostate Hyperplasia). Uvimbe huweza kugawanyika na kukua, na pia hutengeneza mirija mipya ya damu ili kujipatia lishe wenyewe. Kitendo hiki kitaalam huitwa 'Angiogenesis.'

Hata hivyo, uvimbe huu usiokuwa kansa, unaweza kuleta matatizo kama vile kukua sana na kuvibana viungo na tishu nyingine mwilini. Aidha, uvimbe kama huu, huweza kukua na kuingilia mifumo ya umeng'enyaji, fahamu na damu/limfu na huweza kutoa homoni zinazobadili utendaji wa kawaida wa mwili.

Ingawa uvimbe usiokuwa kansa unaweza kuwa hatari kwa afya, lakini hauwezi kuzishambulia seli nyingine au kusambaa katika viungo vingine mwilini. Uvimbe wa aina hii, mara nyingi hutibika na huwa hauhatarishi maisha.

Hata hivyo, aina zote za kansa zina sifa tatu zinazofanana. Sifa hizo ni ukuaji wa seli usiodhibitika, uwezo wa kuvamia na kushambulia tishu nyingine na uwezo wa kusambaa katika viungo vingine mwilini kupitia mishipa ya damu au mikondo ya limfu. Kitendo hicho cha vidudu vua ugonjwa wa kansa kusambaa mwilini kupitia mkondo wa damu na limfu, kitaalam huitwa 'Metastasis

Aina za kansa

Hadi sasa kuna aina zaidi ya 200 za kansa kulingana na kiungo gani cha mwili kimeathirika au eneo la mwili linaloshambuliwa.
Baadhi ya kansa huwashambulia zaidi wanawake, kwa mfano kansa ya matiti na kuna baadhi ambazo huwashambilia zaidi wanaume.

Baadhi ya kansa huwashambulia watu wa kundi fulani katika jamii kutokana na aina yao ya maisha au kazi wanazofanya kila siku, na hali kadhalika kuna baadhi ya kansa au saratani zinazoshambilia watoto zaidi kuliko watu wazima, kwa mfano kansa ya damu aina ya 'Lymphoblastic'.

Zifuatazo ni baadhi ya aina za kansa kulingana na tabia hizo hapo juu:-

CARCINOMAS. Hii ni saratani ambayo hushambulia viungo mbalimbali vya mwili vilivyo ndani na nje, kwa mfano mapafu, matiti, utumbo na kadhalika.
SARCOMAS. Hii ni saratani inayopatikana kwenye mifupa, misuli na tishu mbalimbali mwilini.
LYMPHOMAS. Hii ni saratani zinazoanza kwenye mikondo na vifundo vya limfu na kwenye tishu za kinga ya mwili.
LEUKEMIAS. Hii ni saratani zinazoanza ndani ya ute wa mifupa (bone marrow) na kukusanyika kwenye mishipa ya damu.
ADENOMAS. Hii ni saratani zinazochomoza kwenye tishu na tezi zinazotoa homoni mbalimbali hasa tezi zilizopo kichwani.

Ni nini huchangia kuwepo kwa ugonjwa wa kansa?

Asilimia 60 ya magonjwa yote ya kansa yanahusishwa zaidi na mtindo wa maisha ambao vipengele vyake ni ulaji, mazoezi ya mwili na matumizi ya pombe na tumbaku. Vitu vingine vinavyochangia, ni pamoja na virusi na bakteria, madini mazito, mionzi na sumu kadhaa.

Vyakula huchangia kwa kiasi kikubwa saratani za kinywa na koo, matiti, tezi ya kiume, utumbo mpana, mapafu, tumbo, ini, kongosho na kizazi. Ulaji unaoweza kuchangia ugonjwa huu, ni pamoja na ulaji wa nyama nyekundu kupita kiasi, nyama zilizosindikwa, vyakula vilivyokuzwa kwa kemikali nyingi kama mbolea, vyakula vyenye mafuta mengi ambavyo huweza kusababisha uzito mwingi na vyakula vilivyoota ukungu, kwa mfano karanga.

Kitaalam, nyama nyekundu ni muhimu kwa binadamu, lakini inakuwa tatizo pale inapoliwa zaidi ya nusu kilo kwa wiki. Ulaji wa nyama nyekundu mfano ng'ombe, unaongeza uwezekano wa kupata saratani ya utumbo mkubwa.

Tafiti zimeonesha kuwa kula nyama nyekundu hadi nusu kilo kwa wiki haiongezi uwezekano wa kupata saratani, lakini kila gramu 50 zinazoongezeka, huongeza uwezekano wa kupata saratani kwa asilimia 15.

Nyama zilizosindikwa pamoja na zile zilizohifadhiwa kwa kuongezwa chumvi, mafuta, kemikali au kukaushwa kwa moshi kama nyama za kopo, soseji na bekoni zinaongeza sana uwezekano wa kupata saratani. Hakuna kiasi chochote cha nyama iliyosindikwa kinachoweza kutumika bila kuongeza uwezekano wa kupata saratani.

Viazi vya kukaanga mfano viazi mviringo (ulaya), huongeza hatari ya kupata saratani hasa vikikaangwa kwenye mafuta yenye haidrojeni na lehemu. Viazi ni moja ya vyakula vyenye wanga sana na wakati wa kukaangwa hutoa 'Acrylamide' ambayo ni kisababishi cha  kansa hasa kwenye mfumo wa fahamu.

Vinywaji baridi/Laini  kama vile soda na juisi za viwandani navyo vinaweza kusababisha kansa. Utafiti uliofanywa mwaka 2010 na Jarida la 'Cancer, Epidemiology, Biomakers & Prevention' unaonyesha kuwa mtu aliyetumia soda mbili au zaidi ndani ya wiki moja, ana uwezekano wa kupata saratani ya kongosho kwa asilimia 87 kuliko mtu ambaye hatumii kabisa vinywaji hivyo laini.

Tafiti nyingine zimeonyesha uhusiano kati ya matumizi ya sukari na saratani za tumbo na utumbo mpana, ingawa sukari haifanyi seli nzuri zisizo na kasoro kuwa kansa ila sukari ni chakula ama chanzo cha lishe cha seli za kansa. Pombe na tumbaku. Matumizi ya pombe na tumbaku huchangia sana ongezeko la sarayani za koo na mapafu. Hapa nchini Tanzania, ongezeko ni kubwa kwa sababu ya matumizi ya vitu hivyo.

Kwa mfano, asilimia 90 ya wagonjwa waliopelekwa Hospitali ya Ocean Road, Dar es Salaam, walikuwa na historia ya kutumia vilevi vikali, tumbaku, pilipili kwa wingi na aina nyingine ya vitu vinavyosababisha saratani. Pombe inaongeza sana uwezekano wa kupata saratani hasa zile za koo, kinywa, ini na matiti.

Uzito Uliozidi kiasi unamweka pia mtu kwenye hatari ya kupata magonjwa mengi sugu, kama vile kisukari, msukumo mkubwa wa damu, magonjwa ya moyo, figo, na saratani za matiti, kongosho na kizazi. Utaratibu mzuri wa kula, husaidia kupunguza uzito au kuzuia ongezeko kubwa la mwili.

Virusi na Bakteria husababisha kansa ya ini, mdomo wa mji wa mimba, mdomo, ngozi, tumbo, mfupa wa taya na kibofu cha mkojo. Tabia kama kufanya mapenzi kwa mdomo, kama vile kunyonya uke au uume, huchangia kuenea kwa saratani za iana hiyo.
Ni nini kifanyike kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa huo?

Wataalamu wanashauri kwamba hatari ya kupatwa na kansa inaweza kupungua kwa kubadilisha muundo wa maisha ya mtu binafsi, kwa mfano kujiepusha na uvutaji wa sigara, kujiepusha kukaa juani kwa muda mrefu, kula lishe bora na kufanya mazoezi mara kwa mara.

Aidha, vyakula vitokanavyo na mimea ni kinga nzuri ya kuzuia saratani. Kutumia zaidi vyakula vitokanavyo na mimea husaidia kuondoa uwezekano wa kupata saratani za aina mbalimbali. Inashauriwa kula angalau vipimo vitano vya mboga mbalimbali kwa siku.

Hakikisha katika kila mlo unaotumia kunakuwa na nafaka zisizokobolewa kama vile unga wa ngano usiokobolewa sana, unga wa dona, mchele wa brauni, ulezi na kadhalika na aina mbalimbali za mikunde kama vile maharage, kunde, choroko na mbaazi.
Mazoezi ya mwili yanapaswa kuwa sehemu ya maisha ya kila siku. Inashauriwa kufanya mazoezi ya mwili ya wastani kama vile kutembea haraka haraka angalau dakika 30 kila siku, na mwili ukishazoea, unashauriwa kuongeza hadi kufikia dakika 60 kila siku.
Kama unafanya mazoezi ya nguvu sana, basi iwe angalau dakika 30 kila siku. Punguza sana mtindo wa maisha ambao unakufanya uketi bila mazoezi kama vile kuangalia televisheni kwa muda mrefu.

Tumia nafasi zote zilizopo za kuzoeza mwili kama vile kupanda ngazi badala ya kutumia lifti, kusaidia kazi za nyumbani, kutembea kwenda sokoni au dukani kama si mwendo mrefu na kadhalika.

Nini dalili za ugonjwa wa kansa?

Kwa kawaida saratani huanza taratibu, na huchukua muda mrefu kuonyesha dalili zake zote. Aidha, dalili za awali haziambatani na maumivu yoyote, hivyo kusababisha wagonjwa wengi kuchelewa kutafuta matibabu.

Magonjwa mengi ya saratani hutibika yakigundulika mapema. Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), linaema asilimia 30 ya saratani zinaweza kuzuilika. Hivyo ni muhimu kwa kila mtu kumuona mapema mhudumu wa afya kila anapoona dalili zisizo za kawaida katika mwili wake, kama vile dalili za kutokwa na damu ukeni kwa mwanamke baada ya kufanya tendo la ndoa, baada ya kukoma mzunguko wa hedhi, au nje ya mzunguko wa hedhi.

Kukojoa mara nyingi zaidi ya kawaida au mkojo kutoka kwa shida; uvimbe wa zaidi ya wiki tatu shingoni, kwapani, tumboni, ngozi au matiti; kubadilika kwa kawaida ya kupata choo (kufunga choo); matiti kubadilika umbile, uvimbe, ngozi au kutoa maji maji.
Kukohoa au sauti ya kukwaruza kwa zaidi ya wiki tatu; shida au maumivu wakati wa kumeza chakula au vinywaji; kutokwa na damu kwenye choo, mkojo, makohozi au pua; kutokwa na ute, maji maji au usaha ukeni; uchovu bila kufanya kazi; kupungua uzito ghafla bila sababu na kukosa hamu ya kula chakula.

Jinsi ya kudhibiti kabisa kansa

Ikiwa kansa au saratani ishatokea na kuanza kusambaa mwilini, mambo muhimu yanayopaswa kuzingatiwa ili kudhibiti usambaaji huo ni pamoja na kutibiwa kwa kufanya upasuaji, tiba ikiwemo  (matibabu kwa dawa); kupata matibabu kwa njia ya eksirei (matumizi ya mnururisho wa kuweka ioni ili kuua seli za kansa na kunywea uvimbe); kupata matibabu ya tiba maradhi; kupata matibabu ya monokloni ya kingamwili au njia nyingine