UCHAWI:1



NINI MAANA YA UCHAWI?

Al Azhari ambaye ni
mtungaji wa kamusi
maarafu ya kiarabu iitwayo
“LisanulArab” amesema:
“Neno “Uchawi”, kwa
kiarabu “As Sihr”, maana
yake ni kitendo cha
kujikurubisha na shetani na
kwa msaada wake
(shetani)”, na akasema pia
kuwa; “Uchawi ni
kulibadilisha jambo mbali na
uhakika wake, nako ni
kuwadhihirishia watu jambo
lisilo la kweli wakaliona
kuwa ni la kweli.”
Ama Sahaba Ibni Abbas
(Radhiya Llaahu ‘anhu)
amesema:
"Uchawi ni kuidhirisha batili
katika sura ya haki."
Hayo ni katika kamusi za
lugha.
Amma katika kamusi ya dini,
maana ya neno Uchawi (As
Sihr), kama alivyofasiri
Mwanachuoni mkubwa
Fakhruddin Al Razi kuwa;
"Ni kila jambo lililofichika
sababu zake, linalotokeza
kwa sababu zisizo za
kawaida na ndani yake mna
hadaa (khidaa)."
Amma Sheikh Wahiyd
Abdulsalaam Bali, mwandishi
wa kitabu maarufu
kiitwacho 'Al Saarim Al
Batar fiy muhaarabat Al
Saharatul ashraar', na
kitabu kiitwacho "Al wiqaya
mina l jinni wa shaytan",
ambaye pia ni mtaalamu
maarufu katika elimu ya
majini na mashetani na
uchawi na ambaye pia ni
katika maulamaa maarufu
wanaotoa majini kwa njia ya
kusoma Qur-aan, yeye
anasema:
"Uchawi ni makubaliano
baina ya mchawi na Jinni
akishurutishwa mchawi
kufanya mambo ya haramu
au ya shirki, na baada ya
kufanya hayo, Jinni
anashurutishwa kumsaidia
na kumtii mchawi huyo kwa
kila anachotaka."
Baadhi ya yale ambayo
mchawi anatakiwa na
shetani ayatende ili
ajikurubishe naye ni:
 Mchawi anatakiwa auvae
msahafu miguuni na
aingie nao chooni
 Aandike baadhi ya aya
za Qur-aan kwa damu
ya hedhi.
 Miongoni mwao
wanashurutishwa
kuandika aya za Qur-aan
penye nyayo za miguu.
 Au aiandike suratulFatiha
kinyume nyume.
 Asali bila ya Udhuu.
 Wengine hutakiwa
kuchinja mnyama bila ya
kulitaja jina la
MwenyeziMungu kisha
amtupe mnyama huyo
mahali maalum
anapoamrishwa na
shetani.
 Wamo miongoni mwao
wanaozungumza na
nyota au kuzisujudia.
 Au hutakiwa kuandika
herizi kwa maneno yenye
kufru ndani yake
Imeelezwa kwamba katika
nchi ya Sham kulikuwa na
mtu ambaye watu walikuwa
wakimpenda na kumheshimu
sana wakimdhania kuwa ni
mtu mwenye makarama.
Mtu huyu alikuwa kila
mwaka katika msimu wa
Hajji akiwatumikia watu wa
mji wake kwa kuchukua
barua zao na vitu vyao na
kuwapelekea watu wao
waliokwenda Saudia kuhijji.
www.pilingu.blogspot.com
Alikuwa akipeleka na kurudi
kwa muda wa siku moja au
mbili tu, na watu
walimpenda sana na kuamini
kwamba alikuwa ni Waliy.
Siku moja mtu huyo aliumwa
sana, akamuita mwanawe
na kumwambia kuwa kama
atakufa, basi ende mahali
fulani wakati wa usiku na
atamkuta ngamia wa aina
fulani na ampande na
kufuata amri zote
atakazopewa na ngamia
huyo.
Alipofariki dunia, mwanawe
alifanya kama alivyoambiwa
na baba yake, akaondoka
peke yake wakati wa usiku
na kuelekea jangwani kule
alikoambiwa na baba yake
kuwa atamkuta ngamia.
Akamkuta ngamia kama
alivyoambiwa, akampanda
na alipokuwa akenda,
ngamia akaanza kusema na
kumtaka kijana yule ashuke
na amsujudie.
Yule kijana alistuka sana
kusikia ngamia akisema na
pia akashangazwa na amri
zake, akamwambia:
"Vipi nikusujudie, kweni
wewe ni nani?"
"Ikiwa unataka nifuate amri
zako kama nilivyokuwa kwa
baba yako, na nikupeleke
popote utakapo duniani, basi
unisujudie kama alivyokuwa
akinisujudia baba yako."
Yule kijana akajibu:
"Mimi ninamsujudia
Mwenyezi Mungu peke yake,
amma wewe la, siwezi
kukusujudia."
Ngamia akamrusha kijana
yule kutoka juu ya mgongo
wake na kumwangusha
chini, na kijana yule akatoka
mbio mpaka nyumbani kwa
mama yake na kumuelezea
yote aliyoyaona na kwamba
baba yake alikuwa
akimsujudia Jinni ndiyo
maana alikuwa na uwezo
wa kusafiri kila anapotaka
kwenda kwa kupaishwa na
jini yule.
Kwa haya inatubainikia
kuwa Jinni hamsaidii wala
hamhudumii mchawi wala
mtu yeyote isipokuwa naye
kwa mkabala wake
atumikiwe kwa kutendewa
matendo ya kufru, na
maulamaa wanasema:
"Kila mchawi anapokufuru
zaidi, basi shetani
humtumikia kwa nguvu
zaidi, na mchawi akitaka
apate huduma ya hali ya juu
kabisa kutoka kwa
masultani wa majini au kwa
kiarabu wanaitwa
"Maradatul Jinni", basi
inambidi afanye kufuru
kubwa zaidi, na kwa ajili
hiyo, mchawi anapotaka
nguvu juu ya wenzake
inamlazimikia akufuru zaidi."
Kutokana na haya
tunafahamu kwamba
mchawi na shetani ni
marafiki na washirika katika
kumuasi MwenyeziMungu.
MwenyeziMungu Anasema:
"Na (wakumbushe) siku
atakapowakusanya wote
(akawaambia): "Enyi
makundi ya majini! Hakika
nyinyi mmechukua wafuasi
wengi katika wanaadamu".
Na marafiki wao katika
wanaadamu
(watagombania) waseme:
"Mola wetu! Tulinufaishana
sisi na wao na tumefikia
muda wetu uliotuwekea".
Basi (Mungu) atasema;
"Moto ndio makazi yenu,
mtakaa humo milele", ila
apende MwenyeziMungu
(kuwarehemu), hakika Mola
wako ndiye Mwenye hikima
(na) ndiye ajuaye.”
Al An - Am - 128
Je, Utamjuaje mchawi???
Usipitwe na sehemu ya 2.