HEKIMA YA KULETWA MITUME.

MwenyeziMungu anasema:- "Bila shaka tumempeleka Mtume katika kila umma (awaambie) ya kwamba "Mwabuduni MwenyeziMungu na muepukeni (Iblis) muovu". (An - Nahl -36)

MAISHA YA BARZAKH (BAADA YA KUFA)

MwenyeziMungu anasema: "Hapana! Hakika hili ni neno tu analolisema yeye (aliye mwovu anapofikiwa na mauti) na mbele yao kuna maisha ya baada ya kufa (ya taabu kwa wabaya na ya raha kwa wazuri) mpaka siku watakapofufuliwa!". (Al - Muminun - 100)

VITISHO VYA SIKU YA KIAMA

Na katika kauli Yake:- "(Wakumbusheni) Litakapotokea tokeo (hilo la Kiama). Ambalo kutokea kwake si uwongo. Lifedheheshalo (wabaya). Litukuzalo (wazuri). Ardhi itakapotetemeshwa mtetemeko mkubwa. Na milima itakaposagwa sagwa. Iwe mavumbi yanayopeperushwa". (Al - Waqiah - 1 - 6)

KUMTII MWENYEZIMUNGU NA KUMTII MTUME WAKE(SAW)

MwenyeziMungu anasema:- "Na wenye kumtii MwenyeziMungu na Mtume, basi hao watakuwa pamoja na wale aliowaneemesha MwenyeziMungu; Manabii na Masidiki na Mashahidi na Masalih (watu wema). Na uzuri ulioje (kwa mtu) watu hao kuwa rafiki (zake).” (An - Nisaa -69)

KUTOKA KATIKA DINI -"KUR-TADI"

MwenyeziMungu anasema:- "Wala hawataacha kupigana nanyi, mpaka wakutoeni katika dini yenu, kama wakiweza. Na watakaotoka dini yao katika nyinyi, kisha wakafa hali ya kuwa makafiri, basi hao ndio ambao amali zao zimeharibika katika dunia na akhera. Nao ndio watu wa Motoni. Humo watakaa milele." (Al - Baqarah -217).

FAIDA ZA KIAFYA ZITOKANAZO NA ULAJI WA TENDE.

FAIDA ZA KIAFYA ZITOKANAZO KWA ULAJI WA TENDE. Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, tende ndiyo tunda linaloliwa kwa wingi, pengine kuliko tunda lingine. Pamoja na kuwa ni tunda lenye ladha tamu na nzuri mdomoni, lakini kisayansi pia limethibitika kusheheni madini na vitamini lukuki, hivyo kuwa na faida nyingi kiafya. Nimefanikiwa kukusanyieni faida kumi za tende mwilini nazo ni; 1. Ukila tende mara kwa mara, mwili wako utapata aina mbalimbali za madini na vitamin za kutosha, ambazo zinapatikana kwenye tunda hili maarufu duniani. Katika tende kuna kiasi kidogo tu cha mafuta (fat) na haina lehemu (kolestrol). 2. Ukila tende, utajipatia kiasi cha kutosha cha protini na vitamin B1, B2, B3, B5, A1, na C, virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ustawi wa afya ya mwili wako kwa ujumla. 3. Ulaji wa tende huimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji chakula tumboni, hivyo utaondokana na matatizo ya ukosefu wa choo, au matatizo ya kupata choo kigumu kinachosababisha maumivu wakati wa kujisaidia. Pia ndani ya tende kuna virutubisho vya ‘amino acids’ ambavyo ni muhimu mwilini. 4. Ukila tende, mwili utapata nguvu na kukuondolea uchovu ndani ya nusu saa tu, kwa sababu tende ina virutubisho vya sukari asilia kama vile ‘glucose’, ‘sucrose’ na ‘fructose’. Ili kupata faida zaidi za tende, changanya na maziwa fresh kisha kula. Unapojisikia mchovu, badala ya kunywa vinywaji baridi vinavyodai kuongeza nguvu, kula tende, hata kiasi cha punje tatu kinatosha. Kwa wafunga saumu, ndiyo maana inashauriwa kuanza kufungua kwa kula tende ili kuurejeshea mwili wako nguvu iliyopotea siku nzima. 5. Tende ina madini pia aina ya ‘potassium’ na kiasi kidogo cha chumvi (sodium). Madini haya husaidia uimarishaji wa mishipa ya fahamu. Watafiti wamegundua kwamba ulaji kiasi wa ‘potassium’ huweza kumuepusha mtu na kupatwa na kiharusi (stroke). Pia tende husaidia kupunguza lehemu (cholesterol) mwilini (LDL Cholesterol). 6. Kwa wale wenye matatizo ya ugonjwa wa kukauka damu mwilini (anemia), wanaweza kupata ahueni kwa kula tende kwa wingi ambayo ina kiwango cha kutosha cha madini ya chuma ambayo huhitajika katika utengenezaji wa damu mwilini. Wakati vitu vitamu vingine huozesha meno, utamu wa tende huzuia uozaji wa meno. 7. Kwa tatizo sugu na la muda mrefu la ukosefu wa choo, loweka tende za kutosha kwenye maji kiasi cha lita moja usiku kucha, kisha asubuhi changanya maji hayo pamoja na hizo tende ili upate juisi nzito, kunywa na choo kitafunguka na kuwa laini. 8. Kwa matatizo ya ukosefu wa nguvu za kiume, mchanganyiko maalum wa tende, maziwa, asali na unga wa hiriki vinaweza kuondoa tatizo lako. Chukua kiasi cha kiganja kimoja cha tende, loweka kwenye maziwa ya mbuzi kiasi cha lita moja na yakae usiku kucha. Asubuhi, zisage tende hizo kwenye maziwa hayo hadi zichangayike, kisha weka asali kiasi cha vijiko vitatu au vinne vikubwa pamoja na unga wa hiriki, kiasi cha nusu kijiko kidogo. Kisha kunywa mchangayiko huo kila siku hadi utakapoona mabadiliko ya kuridhisha. 9. Tende ni dawa ya unene, kwa wale wenye matatizo ya wembamba wa kupindukia na wanataka kuongeza uzito, ulaji wa tende kila siku unaweza kuwasaidia. Lakini hii ina maana kwamba, wale wanaohitaji kupunguza uzito, ulaji wa tende kwa wingi hauwezi kuwafaa. Pia tende husaidia uondoaji wa kilevi mwilini. 10. Tende inatibu saratani ya tumbo. Habari njema kuhusu tende kama tiba ni kwamba, haina madhara yoyote kwa sababu ni dawa asilia na inafanyakazi vizuri kuliko dawa za ‘kizungu’. Tende vile vile ina imarisha nuru ya macho na tatizo la kutokuona usiku (night blindness).