HEKIMA YA KULETWA MITUME.

MwenyeziMungu anasema:- "Bila shaka tumempeleka Mtume katika kila umma (awaambie) ya kwamba "Mwabuduni MwenyeziMungu na muepukeni (Iblis) muovu". (An - Nahl -36)

MAISHA YA BARZAKH (BAADA YA KUFA)

MwenyeziMungu anasema: "Hapana! Hakika hili ni neno tu analolisema yeye (aliye mwovu anapofikiwa na mauti) na mbele yao kuna maisha ya baada ya kufa (ya taabu kwa wabaya na ya raha kwa wazuri) mpaka siku watakapofufuliwa!". (Al - Muminun - 100)

VITISHO VYA SIKU YA KIAMA

Na katika kauli Yake:- "(Wakumbusheni) Litakapotokea tokeo (hilo la Kiama). Ambalo kutokea kwake si uwongo. Lifedheheshalo (wabaya). Litukuzalo (wazuri). Ardhi itakapotetemeshwa mtetemeko mkubwa. Na milima itakaposagwa sagwa. Iwe mavumbi yanayopeperushwa". (Al - Waqiah - 1 - 6)

KUMTII MWENYEZIMUNGU NA KUMTII MTUME WAKE(SAW)

MwenyeziMungu anasema:- "Na wenye kumtii MwenyeziMungu na Mtume, basi hao watakuwa pamoja na wale aliowaneemesha MwenyeziMungu; Manabii na Masidiki na Mashahidi na Masalih (watu wema). Na uzuri ulioje (kwa mtu) watu hao kuwa rafiki (zake).” (An - Nisaa -69)

KUTOKA KATIKA DINI -"KUR-TADI"

MwenyeziMungu anasema:- "Wala hawataacha kupigana nanyi, mpaka wakutoeni katika dini yenu, kama wakiweza. Na watakaotoka dini yao katika nyinyi, kisha wakafa hali ya kuwa makafiri, basi hao ndio ambao amali zao zimeharibika katika dunia na akhera. Nao ndio watu wa Motoni. Humo watakaa milele." (Al - Baqarah -217).

FAHAMU UGONJWA WA KANSA DALILI NA TIBA YAKE.

KANSA au kwa jina jingine, Saratani, ni kundi la magonjwa yanayosababishwa na mgawanyiko usio sawa na usiodhibitika wa seli na kuunda uvimbe unaovamia na kuzidhuru tishu za mwilini. Kansa isiyotibiwa, inaweza kuwa ugonjwa unaoshambulia tishu nyingine mwilini na kusababisha kifo. Kwa kawaida, kansa huusababishia mwili madhara pale inapoharibu seli na kuzifanya zigawanyike bila kudhibitika na kuwa uvimbe wa tishu unaojulikana kama tumor, isipokuwa katika kansa ya damu ambapo kansa huzuia utendaji wa kawaida wa damu kwa kuzifanya seli ziwe na mgawanyiko...