HEKIMA YA KULETWA MITUME.

MwenyeziMungu anasema:- "Bila shaka tumempeleka Mtume katika kila umma (awaambie) ya kwamba "Mwabuduni MwenyeziMungu na muepukeni (Iblis) muovu". (An - Nahl -36)

MAISHA YA BARZAKH (BAADA YA KUFA)

MwenyeziMungu anasema: "Hapana! Hakika hili ni neno tu analolisema yeye (aliye mwovu anapofikiwa na mauti) na mbele yao kuna maisha ya baada ya kufa (ya taabu kwa wabaya na ya raha kwa wazuri) mpaka siku watakapofufuliwa!". (Al - Muminun - 100)

VITISHO VYA SIKU YA KIAMA

Na katika kauli Yake:- "(Wakumbusheni) Litakapotokea tokeo (hilo la Kiama). Ambalo kutokea kwake si uwongo. Lifedheheshalo (wabaya). Litukuzalo (wazuri). Ardhi itakapotetemeshwa mtetemeko mkubwa. Na milima itakaposagwa sagwa. Iwe mavumbi yanayopeperushwa". (Al - Waqiah - 1 - 6)

KUMTII MWENYEZIMUNGU NA KUMTII MTUME WAKE(SAW)

MwenyeziMungu anasema:- "Na wenye kumtii MwenyeziMungu na Mtume, basi hao watakuwa pamoja na wale aliowaneemesha MwenyeziMungu; Manabii na Masidiki na Mashahidi na Masalih (watu wema). Na uzuri ulioje (kwa mtu) watu hao kuwa rafiki (zake).” (An - Nisaa -69)

KUTOKA KATIKA DINI -"KUR-TADI"

MwenyeziMungu anasema:- "Wala hawataacha kupigana nanyi, mpaka wakutoeni katika dini yenu, kama wakiweza. Na watakaotoka dini yao katika nyinyi, kisha wakafa hali ya kuwa makafiri, basi hao ndio ambao amali zao zimeharibika katika dunia na akhera. Nao ndio watu wa Motoni. Humo watakaa milele." (Al - Baqarah -217).

TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO (Ulcers).

1. Chemsha habasoda na bizari ya pilau katika maji kunywa kikombe cha chai kutwa x 1
Kila siku kwa miezi 3.

Au
2. Mafuta ya habasoda na habarehani katika maziwa fresh glasi 1 x 3
Kila siku kwa miezi 3.

Au
3. Asali lita1 na unga wa ganda la ndizi vijiko 3 changanya vizuri kisha kula kijiko 1 x 3
Kila siku kwa miezi 3.

Au
4. Ganda la komamanga vijiko 3 na habasoda unga kijiko vijiko 2 tia katika asali lita1 changanya vizuri kisha chota vijiko 2 tia kwenye kikombe 1 cha maziwa kunywa 1x3
Kila siku kwa miezi 3.

Au
5. Kunywa mafuta ya zaituni kijiko 1 na  mafuta ya habasoda kijiko 1 kwenye kikombe 1 cha maji ya moto 1x3 Kila siku kwa miezi 3.

6. Juisi ya karoti na mbatata
Kila siku kwa miezi 3.

www.pilingutz.ga
Au
7.Chukua maganda ya palachichi uyaanike
mpaka yakauke kisha yasage. Chukua unga huo ujazo wa vijiko3 vya chakula pamoja na vijiko 3 vya Asali kisha
tumia kulamba.vijiko 2x3
Kila siku kwa miezi 3.

Au
ASALI NA MDALASINI TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO

Tumia Asali ya nyuki,Mdalasini
na Maji ya Uvuguvugu kila siku
Asubuhi kabla ya
kula kitu na jioni kwa muda wa miezi minne

Namna ya kutengeneza Dawa
fanya hivi:
chukuwa kijiko kikubwa kimoja
cha Asali changanya na kijiko
kimoja cha unga wa
Mdalasini uweke katika Glasi 1
ya Maji ya Uvuguvugu kisha
unywe Asubuhi
kabla ya kula au kunywa kitu
chochote kile na ukae kwa
muda wa saa moja
kupita ndio waweza kula.
Na wakati wa usiku fanya hivyo hivyo kunywa tena
mchanganyiko huo wa Asali na
Unga wa Mdalasini dumisha
hivyo Kila siku kwa miezi 3.
©Sheikh Pilingu Hijama &  Ruqya Center
+255713494945
www.pilingutz.ga

TIBA YA KIHARUSI (KUPOOZA)


1. Soma Ruqya

2. Unga wa Udi karaha vijiko 2, na Habasoda vijiko 2 katika asali lita 1 changanya kisha kula vijiko 2X3 kila siku.

Au
3. Changanya kijiko kimojakimoja cha Bakalhadi, manimani,habatsoda, sufa, makal-arzak, jauza, kakila, udikaraha, ubani maka,ubani dhukra,ubanimashtaka, halilinji, abilinji, tangawizi, hiliki,darufilfili, halititi,basbas jauza. Vyote view ujazo sawa ila sufa izidi changanya na asali lita 1 na siki kikombe 1. Kula kijiko kikubwa 2X3
Mgonjwa avae nguo za kumwongezea joto muda wote.

Au
4.Chemsha kila siku majani ya pakanga kikombe 1 kwenye maji lita 1.
anywe kidogo kidogo  kwa siku mpaka yaishe.

5.kisha umchue sehemu aliyopooza kwa mafuta ya nazi yaliyotiwa Halmiti na irkizamda na karafuu maiti.
1x2.

TIBA YA MARADHI YA FIGO.

1. Kula vijiko 2 vya asali iliyochanganywa na habasoda.
Utie katika glasi ya maji moto.


Au
.2. Kula zabibu kavu 21 kila asubuhi kwa mwezi.

Au
3. Asali lita 1, habasoda unga kijiko1  na thaum kikombe cha kahawa. 
kula kijiko kikubwa 2X3 na kila baada ya chakula kula limao 1.

Au
4. Habasoda kijiko1, harmal kijiko1, Jirjir kijiko1  changanya na asali lita 1.
kula vijiko 2X3 katika maziwa moto siku 7-21

Au
Chemsha ndevu za mahindi ujazo wa lita3
kilasiku kunywa lita moja kwamda wa siku3.
Kama bado utahisi bado ugonjwa upo
kunywatena kwa muda wa siku3.

Au
KUSAFISHA FIGO

Mwaka mpaka mwaka figo zetu zinachuja damu na kuondoa chumvi, sumu, na vitu visivyotakiwa mwilini. Kadiri siku zinavyokwenda chumvi hujirundika katika figo tukio ambalo ni hatarishi katika mfumo bora wa utendekazi wa figo hivyo kufanya uhitaji figo kusafishwa mara kwa mara.

NAMNA YAKUSAFISHA FIGO

Ni rahisi sana, kwanza chukua kiasi cha majani ya 'kotimiri' (parsley) au majani ya 'dhania' (coriander) kiasi cha vifungo viwili kisha yaoshe vizuri, katakata katika vipisi vikubwa kubwa kisha weka kwenye chombo ambacho utaweza kuchemshia kama vile sufuria.  Weka maji (lita moja) katika sufuria yenye majani hayo kisha chemsha kwa muda was dakika kumi, iache ipoe kisha chuja vizuri na uweke kwenye chupa kisha uiweke katika jokofu ili iweze kupoa zaidi na kupata ubaridi.

Kunywa glasi moja kila siku kama umetumia dhania na utaona  chumvi na vitu vyote vilivyorundikana kwenye figo vinatoka kwenye mkojo wakati unapojisaidia haja ndogo, pia utahisi utofauti katika mwili wako ambao hujawahi kuuhisi. Kama utatumia majani ya parsley (kotimiri)  usikunywe zaidi ya vijiko vinne vya mezani.

- Ukitumia majani ya dhania kunywa glasi moja kila siku
- Ukitumia majani ya parsley(kotimiri)  vijiko vinne vya mezani vya maji ile kila siku na usinywe kama hujakula

Kotimiri pamoja na majani ya dhania yanafahamika kwa uwezo wao bora wakusafisha figo na pia hizi zenyewe ni za asili zote. Zinatoa matokeo sawa pale zinapotumika kusafisha figo, lakini majani ya kotimiri (parsley) yanapendelewa zaidi na ni chaguo zuri kwasababu ya utofauti wake na majani ya dhania (coriander).

Utofauti uliopo Kati ya kotimiri na majani ya dhania ni kwamba; Majani ya kotimiri hayana harufu yoyote ila majani ya dhania yana harufu, pia majani ya kotimiri yanatumika sana kutengenezea saladi. Japo majani haya yanafanana sana ukiangalia kwa ukaribu na kwa makini utagundua kuwa yana utofauti.

ANGALIZO

Juisi hii ya kotimiri ina nguvu sana hivyo usiinywe bila kuwa na kitu tumboni yani ule kwanza kabla yakutumia hii juice, pia usinywe zaid ya mililita 30 yani kipimo kiasi cha vijiko vinne vikubwa vya meza kwa siku. Chukua uangalizi wa karibu wa kujitathimini kama ni mara yako ya kwanza kusafisha figo zako.

Mama mjamzito asitumie juisi hii.

Kotimiri inaaminika kuwa nakiwango kikubwa cha asidi inaitwa 'oxalic acid' hivyo kwa mtu mwenye tatizo la mawe kwa figo asitumie bila ushauri wa docta wa tiba za asili, yani kwa ufasihi mwenye vijiwe katika figo lazima aitumie kwa uangalifu wa daktari kwa ni tiba pia ya kuyayusha hizo vijiwe na kuna vipimo tafauti vitahitajika, pia usitumie na vyakula vingine vyenye madini ya calcium kwani madini ya calcium pamoja na asidi ya oxalic ikichanganyika inageuza ile dawa isiwe organic.

+255713494945 

JE UNAJUWA KIUNGULIA NI NINI?

KIUNGULIA NA TIBA YAKE. 

Kiungulia (heart burn) ni hali ya kuckia kama unaungua ndan ya koo nayo ni baada ya fluid (HCL acid) ilioko tumbon kupanda kwenye mrija wa chakula (oesophagus) hutokana na kula vyakula vya wanga kwa wingi (starch) na gesi ni hewa tu ambayo mara nyng hua inajaa tumboni huweza sababishwa na wadudu wanao act ktk chakula na kutoa gesi kama ni moja ya product zake hata helicobacta pylory anaesababisha vidonda va tumbo husababisha ges na kuhc tumbo limejaaa



HCL ktk tumbo huzalishwa na parietal cells ambazo ni moja kati ya aina kuu mbili za cell zinazo tanda ktk tezi za tumbo

Huzalishwa baada ya kuckia chakula au kufika mda wa mtu hyo wa kula, hua ni moja ya content ya gastric juic (isaidiayo ktk kumeng'enya chakula)

TIBA YAKE. 


1. Kijiko kimoja cha habasoda katika glasi moja ya maziwa kutwa x 3



2. Au chota kijiko 1 cha unga wa Shimari kula 1x4 kila siku au kila baada ya kula. 

Kisha utamalizia kwa kunywa maji ya vuguvugu. 

©

Sheikh Pilingu Hijama & Ruqya Center
+255713494945

YAJUWE MAMBO 10 YANAYOHARIBU FIGO.

Kwa kifupi sana leo tunakutajia baadhi ya Tabia zinazochangia kuharibika kwa Figo. Tutambue kuwa tatizo hili la kufeli kwa figo limeshawakumba wengi na baadhi yao wameshapoteza maisha.
Ukiwa mzima mshukuru Mungu na ni vyema ukasoma makala hii ili kujinusuru na janga hili la kuharibikiwa figo.
Hizi hapa ni baadhi ya tabia 10 zinazoharibu figo:
1. Kubana mkojo kwa muda mrefu
2. Kutokunywa maji ya kutosha
3. Kutumia chumvi nyingi
4. Kula nyama mara nyingi zaidi
5. Kutokula chakula cha kutosha
6. Kuchelewa kujitibu maambukizi madogomadogo
7. Kutumia visivyo dawa za maumivu
8. Utumiaji wa madawa kwa ajili ya Insulin
9. Kunywa pombe kupita kiasi
10. Kutopata muda wa kutosha kupumzika

Ukiwa na tatizo la Figo njoo upate tiba sahihi na ushauri kituoni kwetu Sheikh Pilingu Ruqya &  Hijama Center
Au piga simu 0713494945
Email: pilingurashidi@gmail.com

WENGU KUVIMBA MWILI


1. DUA

Au
2. changanya unga wa Hulba na natrun au Khardali pamoja na siki- paka

Au
3. habasoda na siki ya Zabibu chemsha kisha paka kwenye uvimbe na ule vijiko 2X3

DAWA YA NGOZI. (Mba, upele, Chunusi, Fangasi, Miwasho, Malengelenge, Mapunye, Utangotango n.k.


1. Mafuta ya habasoda changanya na mafuta ya waridi na ngano nyukundu- vyote ujazo sawa ila ngano izidi kisha upake kutwa X2 au soma 1:1 au 57:4

KUUNGUA MOTO
2. Ngozi iliyoteketea kwa moto paka asali iliyo changanywa na ute wa yai.

FANGASI
3. Kibiritu azraqu na aswfaru na maziwa ya cowball na mafuta paka kutwa X2

4.Changanya sufa na asali na unywe kijiko 1X3

5.Soma dawa namba 9

6.Changanya mafuta ya H.soda na mafuta ya wardi na ngano nyekundu. Vyote ujazo sawa ila ngano iweX2 paka kutwa X2

NGOZI ILIYOTEKETEA KWA MOTO

7.Changanya asali na ute wa yai kasha paka.

8.Changanya maziwa ya Cowbell na Kibritu aswataru na mafuta yoyote. Paka X2

FANGASI BAINA YA MAPAJA
9.Paka mafuta ya H.saoda kabla ya kulala. Siku 7

10.Majani ya Mrehani sugua kichwani pia hutunza nywele kung’oka na na kuzifanya ziwe nyeusi

11.Changanya mafuta ya Habasoda na mafuta ya Zaituni paka pale palipo athirika

12.Changanya kwa ujazo sawa mafuta ya Habasoda Mafuta ya Mdarasini, mafuta ya Ndimu na Mafuta ya Kitunguu Thaumu.
Chemsha kisha paka kutwa x2.

UTAMJUAJE MTU ALIYEATHIRIKA NA UCHAWI AU MAJINI?.


1.  Kuumwa kichwa upande mmoja,meno,mgongo,kiuno na kubanwa kifua.
2.  Kuumwa tumbo chini ya kitovu hii ni kwa akinamama.
3.  Moyo kwenda mbio na kushtuka bila asbabu.
4.  Kushika moto mwili hasa miguu pmj na ganzi na maumivu makali.
5.  Kizunguzungu mara kwa mara.
6.  Kuumwa tumbo sana kwa akinamama wakati wa period pmj na kutoa damu nyingi au chache sana.
7.  Kupata maumivu makali wakati wa jimai kwa akinamama na kukosa hamu ya tendo hilo au kulichukia kabithaaaa.
8.  Kutembelewa na vitu mwilini.
9.  Kutingishika,kutetemeka sana na kulia bila sababu ikiwemo na hasira sana.
10.  Kuhisi uzito wa mwili kana kwamba umebeba mzigo mzito.
11.  Chuki ndani ya ndoa kutamani kuachwa au kuacha bila asbabu.
12.  Maneno machafu kwa mwenza na punde tyuu majuto mjukuu.
13.  Kufungika hedhi bila sababu na kutoshika ujauzito bila sababu za msingi.
14.  Kuota umjauzito,unazaa,unanyonyesha na unabeba watoto.
15.  Kujaa kitumbo ndiiii bila ujauzito na kuchezacheza kitu tumboni bila ya ujauzito.
16.  Kuharibika mimba baada ya kuota unafanya vituuuuz na mtu atishae au hata umjuae au usiyomjua.
17.  Kuyeyuka na kuharibika mimba bila sababu za msingi.
18.  Ndoto za jimai mara kwa mara.
19.  Kuwa na hamu sana ya mambo yetu yaleeeeeee uwapo peke yako lkn ukutanapo na mwenza hamu hiyooooo ishasepa na kwa mume hupotelewa na nguvu ghafla.
20.  Kuvurugika mipango ya kuoa au kuolewa mara kwa mara.
21.  Kuhisi unaingiliwa au kuingilia babaweeeee hii sio ndotonivyoooooo uvitambue babaaaaaa.
22.  Kutopenda ibadah lkn maasi unayapa mahabba mazitooo.
23.  Hasira,uvivu pmj na hofu bila sababu.
24.  Kuhisi kusimamiwa na mtu mbele yako,nyuma,pembeni na hata ulalapo na kuwa na hofu sana juu ya hilo.
25.  Kukosa usingizi au usingizi mzito mpk swalat subhi ikakupita.
26.  Usomapo Qur-an au kusikiliza hotuba ya ijumaa hupata usingizi a.k.a kusinziasinzia lkn usomapo magazeti au mazungumzo mengine usingizi hauji ng'oooo.
27.  Tamaa kupita kiasi na kujihisi ni mtu wa thamani sana kinyume na ulivyo.
28.  M/mke kupenda kujiremba awapo nje ya nyumba yake lkn akiwa ndani kwake huwa hajirembi na km ana mume basi hubaki kumuachia harufu mbaya mumewe. loh wanawake nyiyeeee loh hebu jirembeni mkiwa ndani ili sisi waume zenu tujihisi kupendwa nasi tukazidisha upendo.
29.  Kupenda vitu vya upuuzi km vile miziki,porojo,udaku,vipindi vya TV visivyo na maana au redio.
30.  Kuota ndoto za vitisho km vile wanyama wakali,au unafanyiwa uadui au unazingirwa na maji,kifo,jeneza,unatumbukia shimoni na unapaa hewani wala mbawa hauna.
31.  Kuota ibada zisizo na mwelekeo.
32.  Kulia,kucheka na kupiga kelele usingizini a.k.a Jinamizi.
33.  Kuchanganyikiwa ndani ya swala pmj na kuyumba na kusinzia usiisahauvyooo.
34.  Kuota mtu mfu au unaelezwa jambo ndotoni na ikiwa yote ni kweli hali hauna Uchamungu na hivyo.
35.  Kuota watu watishao.
36.  Kuota sana nyumba za ibada (misikiti)hali wewe si mtu wa ibada.
37.  Kuota unafanya mashauri na watuwafu a.k.a Mizimuuu.
38.  Kuota unafanyiwa shughuli zote za mazishi au unamfanyia mwenzio.
39.  Kuota unaingiliwa au unaingilia kinyume na maumbile a.k.a Liwatwi.
40.  Kushtukashtuka mara kwa mara usingizini.
41.  Kuibiwa pesa hata uzifungie waaaaapi vileeeee a.k.a Chumaulete.
Haya ndg zangu hizo ndio dalili 41 nilizosema nitawaekea na zipo nyingi zote hizo zinaashiria mtu kusumbuliwa na shetani wa kijini (wachawi) na mtu sio lzm awe nazo zote

AAYAATUL BASWARI


Ni aya ambazo unaweza kumsomea Mgonjwa yoyote wa Macho yanayo uma, uhafifu wa kuona, kutoa uchafu, kutoa machozi, kuona giza kukereketa, kuchonyota n.k.
Msomee kutwa x2
Bi-idhnillaahi anaweza kupona bila bila kumpa kitu chengine.

(وَلَتَجِدَنَّهُمْ أَحْرَصَ النَّاسِ عَلَىٰ حَيَاةٍ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا ۚ يَوَدُّ أَحَدُهُمْ لَوْ يُعَمَّرُ أَلْفَ سَنَةٍ وَمَا هُوَ بِمُزَحْزِحِهِ مِنَ الْعَذَابِ أَنْ يُعَمَّرَ ۗ وَاللَّهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ)
[Surat Al-Baqarah 96]

(وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنْفُسِكُمْ مِنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِنْدَ اللَّهِ ۗ إِنَّ اللَّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ)
[Surat Al-Baqarah 110]

(وَالْوَالِدَاتُ يُرْضِعْنَ أَوْلَادَهُنَّ حَوْلَيْنِ كَامِلَيْنِ ۖ لِمَنْ أَرَادَ أَنْ يُتِمَّ الرَّضَاعَةَ ۚ وَعَلَى الْمَوْلُودِ لَهُ رِزْقُهُنَّ وَكِسْوَتُهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ لَا تُكَلَّفُ نَفْسٌ إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَا تُضَارَّ وَالِدَةٌ بِوَلَدِهَا وَلَا مَوْلُودٌ لَهُ بِوَلَدِهِ ۚ وَعَلَى الْوَارِثِ مِثْلُ ذَٰلِكَ ۗ فَإِنْ أَرَادَا فِصَالًا عَنْ تَرَاضٍ مِنْهُمَا وَتَشَاوُرٍ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا ۗ وَإِنْ أَرَدْتُمْ أَنْ تَسْتَرْضِعُوا أَوْلَادَكُمْ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِذَا سَلَّمْتُمْ مَا آتَيْتُمْ بِالْمَعْرُوفِ ۗ وَاتَّقُوا اللَّهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ)
[Surat Al-Baqarah 233]

(وَإِنْ طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِنْ قَبْلِ أَنْ تَمَسُّوهُنَّ وَقَدْ فَرَضْتُمْ لَهُنَّ فَرِيضَةً فَنِصْفُ مَا فَرَضْتُمْ إِلَّا أَنْ يَعْفُونَ أَوْ يَعْفُوَ الَّذِي بِيَدِهِ عُقْدَةُ النِّكَاحِ ۚ وَأَنْ تَعْفُوا أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۚ وَلَا تَنْسَوُا الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ)
[Surat Al-Baqarah 237]

(وَمَثَلُ الَّذِينَ يُنْفِقُونَ أَمْوَالَهُمُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّهِ وَتَثْبِيتًا مِنْ أَنْفُسِهِمْ كَمَثَلِ جَنَّةٍ بِرَبْوَةٍ أَصَابَهَا وَابِلٌ فَآتَتْ أُكُلَهَا ضِعْفَيْنِ فَإِنْ لَمْ يُصِبْهَا وَابِلٌ فَطَلٌّ ۗ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ)
[Surat Al-Baqarah 265]

(قُلْ أَؤُنَبِّئُكُمْ بِخَيْرٍ مِنْ ذَٰلِكُمْ ۚ لِلَّذِينَ اتَّقَوْا عِنْدَ رَبِّهِمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَأَزْوَاجٌ مُطَهَّرَةٌ وَرِضْوَانٌ مِنَ اللَّهِ ۗ وَاللَّهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ)
[Surat Aal-E-Imran 15]

(فَإِنْ حَاجُّوكَ فَقُلْ أَسْلَمْتُ وَجْهِيَ لِلَّهِ وَمَنِ اتَّبَعَنِ ۗ وَقُلْ لِلَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْأُمِّيِّينَ أَأَسْلَمْتُمْ ۚ فَإِنْ أَسْلَمُوا فَقَدِ اهْتَدَوْا ۖ وَإِنْ تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا عَلَيْكَ الْبَلَاغُ ۗ وَاللَّهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ)
[Surat Aal-E-Imran 20]

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ كَفَرُوا وَقَالُوا لِإِخْوَانِهِمْ إِذَا ضَرَبُوا فِي الْأَرْضِ أَوْ كَانُوا غُزًّى لَوْ كَانُوا عِنْدَنَا مَا مَاتُوا وَمَا قُتِلُوا لِيَجْعَلَ اللَّهُ ذَٰلِكَ حَسْرَةً فِي قُلُوبِهِمْ ۗ وَاللَّهُ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۗ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ)
[Surat Aal-E-Imran 156]

(هُمْ دَرَجَاتٌ عِنْدَ اللَّهِ ۗ وَاللَّهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ)
[Surat Aal-E-Imran 163]

(إِنَّ اللَّهَ يَأْمُرُكُمْ أَنْ تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا وَإِذَا حَكَمْتُمْ بَيْنَ النَّاسِ أَنْ تَحْكُمُوا بِالْعَدْلِ ۚ إِنَّ اللَّهَ نِعِمَّا يَعِظُكُمْ بِهِ ۗ إِنَّ اللَّهَ كَانَ سَمِيعًا بَصِيرًا)
[Surat An-Nisa' 58]

(مَنْ كَانَ يُرِيدُ ثَوَابَ الدُّنْيَا فَعِنْدَ اللَّهِ ثَوَابُ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۚ وَكَانَ اللَّهُ سَمِيعًا بَصِيرًا)
[Surat An-Nisa' 134]

(وَحَسِبُوا أَلَّا تَكُونَ فِتْنَةٌ فَعَمُوا وَصَمُّوا ثُمَّ تَابَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ ثُمَّ عَمُوا وَصَمُّوا كَثِيرٌ مِنْهُمْ ۚ وَاللَّهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ)
[Surat Al-Ma'idah 71]

(وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ كُلُّهُ لِلَّهِ ۚ فَإِنِ انْتَهَوْا فَإِنَّ اللَّهَ بِمَا يَعْمَلُونَ بَصِيرٌ)
[Surat Al-Anfal 39]
(إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنْفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالَّذِينَ آوَوْا وَنَصَرُوا أُولَٰئِكَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يُهَاجِرُوا مَا لَكُمْ مِنْ وَلَايَتِهِمْ مِنْ شَيْءٍ حَتَّىٰ يُهَاجِرُوا ۚ وَإِنِ اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ إِلَّا عَلَىٰ قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُمْ مِيثَاقٌ ۗ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ)
[Surat Al-Anfal 72]

(فَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ وَمَنْ تَابَ مَعَكَ وَلَا تَطْغَوْا ۚ إِنَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ)
[Surat Hud 112]

(اذْهَبُوا بِقَمِيصِي هَٰذَا فَأَلْقُوهُ عَلَىٰ وَجْهِ أَبِي يَأْتِ بَصِيرًا وَأْتُونِي بِأَهْلِكُمْ أَجْمَعِينَ)
[Surat Yusuf 93]

(فَلَمَّا أَنْ جَاءَ الْبَشِيرُ أَلْقَاهُ عَلَىٰ وَجْهِهِ فَارْتَدَّ بَصِيرًا ۖ قَالَ أَلَمْ أَقُلْ لَكُمْ إِنِّي أَعْلَمُ مِنَ اللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ)
[Surat Yusuf 96]

(فَلَمَّا أَنْ جَاءَ الْبَشِيرُ أَلْقَاهُ عَلَىٰ وَجْهِهِ فَارْتَدَّ بَصِيرًا ۖ قَالَ أَلَمْ أَقُلْ لَكُمْ إِنِّي أَعْلَمُ مِنَ اللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ)
[Surat Yusuf 96]

(قُلْ هَٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي ۖ وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ)
[Surat Yusuf 108]

(وَكَمْ أَهْلَكْنَا مِنَ الْقُرُونِ مِنْ بَعْدِ نُوحٍ ۗ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ بِذُنُوبِ عِبَادِهِ خَبِيرًا بَصِيرًا)
[Surat Al-Isra' 17]

(إِنَّ رَبَّكَ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَنْ يَشَاءُ وَيَقْدِرُ ۚ إِنَّهُ كَانَ بِعِبَادِهِ خَبِيرًا بَصِيرًا)
[Surat Al-Isra' 30]

(قُلْ كَفَىٰ بِاللَّهِ شَهِيدًا بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۚ إِنَّهُ كَانَ بِعِبَادِهِ خَبِيرًا بَصِيرًا)
[Surat Al-Isra' 96]

(إِنَّكَ كُنْتَ بِنَا بَصِيرًا)
[Surat Ta-Ha 35]

(قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَىٰ وَقَدْ كُنْتُ بَصِيرًا)
[Surat Ta-Ha 125]

(ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّهَ يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ وَأَنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ)
[Surat Al-Hajj 61]

(اللَّهُ يَصْطَفِي مِنَ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا وَمِنَ النَّاسِ ۚ إِنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ)
[Surat Al-Hajj 75]

(وَمَا أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ مِنَ الْمُرْسَلِينَ إِلَّا إِنَّهُمْ لَيَأْكُلُونَ الطَّعَامَ وَيَمْشُونَ فِي الْأَسْوَاقِ ۗ وَجَعَلْنَا بَعْضَكُمْ لِبَعْضٍ فِتْنَةً أَتَصْبِرُونَ ۗ وَكَانَ رَبُّكَ بَصِيرًا)
[Surat Al-Furqan 20]

(مَا خَلْقُكُمْ وَلَا بَعْثُكُمْ إِلَّا كَنَفْسٍ وَاحِدَةٍ ۗ إِنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ)
[Surat Luqman 28]

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ جَاءَتْكُمْ جُنُودٌ فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا وَجُنُودًا لَمْ تَرَوْهَا ۚ وَكَانَ اللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرًا)
[Surat Al-Ahzab 9]

(أَنِ اعْمَلْ سَابِغَاتٍ وَقَدِّرْ فِي السَّرْدِ ۖ وَاعْمَلُوا صَالِحًا ۖ إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ)
[Surat Saba' 11]

(أَنِ اعْمَلْ سَابِغَاتٍ وَقَدِّرْ فِي السَّرْدِ ۖ وَاعْمَلُوا صَالِحًا ۖ إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ)
[Surat Saba' 11]

(وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ مِنَ الْكِتَابِ هُوَ الْحَقُّ مُصَدِّقًا لِمَا بَيْنَ يَدَيْهِ ۗ إِنَّ اللَّهَ بِعِبَادِهِ لَخَبِيرٌ بَصِيرٌ)
[Surat Fatir 31]
(وَلَوْ يُؤَاخِذُ اللَّهُ النَّاسَ بِمَا كَسَبُوا مَا تَرَكَ عَلَىٰ ظَهْرِهَا مِنْ دَابَّةٍ وَلَٰكِنْ يُؤَخِّرُهُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُسَمًّى ۖ فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ فَإِنَّ اللَّهَ كَانَ بِعِبَادِهِ بَصِيرًا)
[Surat Fatir 45]

(فَسَتَذْكُرُونَ مَا أَقُولُ لَكُمْ ۚ وَأُفَوِّضُ أَمْرِي إِلَى اللَّهِ ۚ إِنَّ اللَّهَ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ)
[Surat Ghafir 44]

(إِنَّ الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي آيَاتِنَا لَا يَخْفَوْنَ عَلَيْنَا ۗ أَفَمَنْ يُلْقَىٰ فِي النَّارِ خَيْرٌ أَمْ مَنْ يَأْتِي آمِنًا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ اعْمَلُوا مَا شِئْتُمْ ۖ إِنَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ)
[Surat Fussilat 40]

(وَلَوْ بَسَطَ اللَّهُ الرِّزْقَ لِعِبَادِهِ لَبَغَوْا فِي الْأَرْضِ وَلَٰكِنْ يُنَزِّلُ بِقَدَرٍ مَا يَشَاءُ ۚ إِنَّهُ بِعِبَادِهِ خَبِيرٌ بَصِيرٌ)
[Surat Ash-Shura 27]

(وَهُوَ الَّذِي كَفَّ أَيْدِيَهُمْ عَنْكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ عَنْهُمْ بِبَطْنِ مَكَّةَ مِنْ بَعْدِ أَنْ أَظْفَرَكُمْ عَلَيْهِمْ ۚ وَكَانَ اللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرًا)
[Surat Al-Fath 24]

(إِنَّ اللَّهَ يَعْلَمُ غَيْبَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَاللَّهُ بَصِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ)
[Surat Al-Hujurat 18]

(هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنْزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا ۖ وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنْتُمْ ۚ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ)
[Surat Al-Hadid 4]

(بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ قَدْ سَمِعَ اللَّهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا وَتَشْتَكِي إِلَى اللَّهِ وَاللَّهُ يَسْمَعُ تَحَاوُرَكُمَا ۚ إِنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ)
[Surat Al-Mujadila 1]

(لَنْ تَنْفَعَكُمْ أَرْحَامُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ ۚ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يَفْصِلُ بَيْنَكُمْ ۚ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ)
[Surat Al-Mumtahana 3]

(هُوَ الَّذِي خَلَقَكُمْ فَمِنْكُمْ كَافِرٌ وَمِنْكُمْ مُؤْمِنٌ ۚ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ)
[Surat At-Taghabun 2]

(أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَى الطَّيْرِ فَوْقَهُمْ صَافَّاتٍ وَيَقْبِضْنَ ۚ مَا يُمْسِكُهُنَّ إِلَّا الرَّحْمَٰنُ ۚ إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ بَصِيرٌ)
[Surat Al-Mulk 19]

(أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَى الطَّيْرِ فَوْقَهُمْ صَافَّاتٍ وَيَقْبِضْنَ ۚ مَا يُمْسِكُهُنَّ إِلَّا الرَّحْمَٰنُ ۚ إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ بَصِيرٌ)
[Surat Al-Mulk 19]

(بَلِ الْإِنْسَانُ عَلَىٰ نَفْسِهِ بَصِيرَةٌ)
[Surat Al-Qiyamah 14]

(إِنَّا خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ مِنْ نُطْفَةٍ أَمْشَاجٍ نَبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَاهُ سَمِيعًا بَصِيرًا)
[Surat Al-Insan 2]

(وَاللَّيْلِ وَمَا وَسَقَ)
[Surat Al-Inshiqaq 17]

(بَلَىٰ إِنَّ رَبَّهُ كَانَ بِهِ بَصِيرًا)
[Surat Al-Inshiqaq 15]

TATIZO LA MINYOO.


1. Chemsha Qusti kunywa.

2. Asali glasi moja na habasoda ya unga kijiko1  na thaumu kijiko1 changanya. kula vijiko 3x3.

Au
3 tumia kitunguu thaumu.
KITUNGUU SWAUMU NI DAWA YA MARADHI ZAIDI YA 30

HARUFU ICHOMAYO.
Ili kuepukana na harufu ya kitunguu swaumu baada
ya kukila kula tofaa au tafuna majani mabichi ya
naanaa, au kunywa maji yaliyotokosewa karafuu. Kitunguu swaumu kitapoteza nguvu ya tiba
iwapo kitapikwa na kila kinapowekwa muda mrefu
ndipo nguvu zake huongezeka (baada ya majani
yake kukauka kabisa).
Kitunguu swaumu kimekusanya protin 49%,sulphur
25%,kiasi fulani cha chumvi,
Homoni zitoazo nguvu
za kiume,viuaji sumu, vikojozavyo, vitoavyo
safura, vinavyoteremsha hedhi, vimeng'enyo vyenye
kuyeyusha mafuta na viini vyenye kuua minyoo.
Kila utafiti unapoendelea ndipo faida na maajabu ya
kitunguu swaumu yanapoongezeka.

www.pilingu.blogspot.com

BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIWA NA
KITUNGUU SWAUMU;

1.Kiua sumu
2.Kisafisha tumbo
3.Kiyeyusha mafuta(cholestro)
4.Huzuia mvilio wa damu
5.Kusafisha njia ya mkojo
6.Kutibu amoeba
7.Kuzuia kuhara damu(Dysentery)
8.Tumbo kushindwa kumeng'enya(Indigestion)
9.Gesi
10.Msokoto wa tumbo
11.Typhoid
12.Kidonda kilichooza
13.Dondakoo
14.Mabaka
15.Baridi yabisi(Rheumatisim)
16.Mishipa
17.Uziwi
18.Virusi vya homa ya mafua(Influenza)
19.Mafua
20.Saratani(Cancer)
21.Kifaduro
22.Kifua kikuu cha mapafu
23.Kipindupindu
24.Kutoa minyoo
25.Upele
26.Kuvunjavunja mawe katika figo
27.Mba kichwani
28.Kuupa nguvu ubongo
29.Kuupa nguvu fizi
30.Kuzuia meno kung'ooka
31.Nguvu za kiume
32.Maumivu ya kichwa
33.Kizunguzungu/kisunzi
34.Kutuliza maumivu ya meno
35.Kujenga misuli na kutia nguvu
36.Mkakamo wa ateri(Arteriosclerosis)
37.Shinikizo la damu
38.Kinga ya tauni na ukimwi
39.Magonjwa ya macho

MATUMIZI NA MAANDALIZI KATIKA KUTIBU

Matumizi na maandalizi ya kitunguu swaumu.
Namna nzuri ni kukisaga kitunguu kikombe 1 kwenye Maji lita 1. Kunywa kikombe 1 cha kahawa x3 kila siku.

Kikipikwa
kinapoteza nguvu ya tiba kutegemeana na tiba
unayokusudia.
Kumbuka pia kwamba kitunguu swaumu huweza
kuchanganywa na vitu vingine
mfano;maziwa,asali,habatsouda,juisi,shayiri.nk.

15. KUFUNGUWA MAZIWA ILI YATOKE.

1. Changanya asali lita 1 na habasoda ya unga kijiko1  na ya  mafuta kijiko 1
Kunywa vijiko 2 kutwa x3

Au
2. Chemsha hulba ya Unga kijiko1 maji lita 1 pilipili nyeupe kijiko1.
kunywa kikombe 1x3 kwa siku 7.