HEKIMA YA KULETWA MITUME.

MwenyeziMungu anasema:- "Bila shaka tumempeleka Mtume katika kila umma (awaambie) ya kwamba "Mwabuduni MwenyeziMungu na muepukeni (Iblis) muovu". (An - Nahl -36)

MAISHA YA BARZAKH (BAADA YA KUFA)

MwenyeziMungu anasema: "Hapana! Hakika hili ni neno tu analolisema yeye (aliye mwovu anapofikiwa na mauti) na mbele yao kuna maisha ya baada ya kufa (ya taabu kwa wabaya na ya raha kwa wazuri) mpaka siku watakapofufuliwa!". (Al - Muminun - 100)

VITISHO VYA SIKU YA KIAMA

Na katika kauli Yake:- "(Wakumbusheni) Litakapotokea tokeo (hilo la Kiama). Ambalo kutokea kwake si uwongo. Lifedheheshalo (wabaya). Litukuzalo (wazuri). Ardhi itakapotetemeshwa mtetemeko mkubwa. Na milima itakaposagwa sagwa. Iwe mavumbi yanayopeperushwa". (Al - Waqiah - 1 - 6)

KUMTII MWENYEZIMUNGU NA KUMTII MTUME WAKE(SAW)

MwenyeziMungu anasema:- "Na wenye kumtii MwenyeziMungu na Mtume, basi hao watakuwa pamoja na wale aliowaneemesha MwenyeziMungu; Manabii na Masidiki na Mashahidi na Masalih (watu wema). Na uzuri ulioje (kwa mtu) watu hao kuwa rafiki (zake).” (An - Nisaa -69)

KUTOKA KATIKA DINI -"KUR-TADI"

MwenyeziMungu anasema:- "Wala hawataacha kupigana nanyi, mpaka wakutoeni katika dini yenu, kama wakiweza. Na watakaotoka dini yao katika nyinyi, kisha wakafa hali ya kuwa makafiri, basi hao ndio ambao amali zao zimeharibika katika dunia na akhera. Nao ndio watu wa Motoni. Humo watakaa milele." (Al - Baqarah -217).

MADHARA YA ZINAA KISAYANSI. Wengi katika wanadamu wanajaribu kuhoji kwa nini Mwenyezi Mungu anakataza zinaa wakati kuingiliana baina


MADHARA YA ZINAA KISAYANSI

Wengi katika wanadamu wanajaribu
kuhoji kwa nini Mwenyezi Mungu
anakataza zinaa wakati kuingiliana baina
ya mke na mume na kuingiliana baina
ya hawara na hawara mambo ni yale
yale, sasa kwa nini akataze??? Kwanza
ifahamike kwamba Mwenyezi Mungu
akikataza jambo basi ujue lina hasara
kwetu kwa kulifuata na lina faida kubwa
kama tukiliacha. Tofauti na wanadamu,
kwa mfano; Serikali inakataza pombe
ya Gongo kwa madai kuwa ni haramu
wakati Bia pia ni pombe lakini ni halali!
Hiyo ni kwa mujibu wa serikali za
ulimwengu. Lakini katika UISLAMU
Mwenyezi Mungu akisema pombe ni
haramu basi iwe Gongo,Bia,n.k zote ni
HARAMU. Ndivyo pia ilivyo ZINAA, leo
ulimwenguni kuna zinaa ya halali
wenyewe wanaita “zinaa salama ya
kutumia Condom” lakini uislamu
umeharamisha kabisa zinaa, iwe ya
Condom au bila Condom huo ndio
uislamu na ndiyo amri za Mwenyezi
Mungu.
Mwenyezi Mungu anasema katika
Qur’an, sura ya 17 Bani Israil aya ya
32;
“Na wala msiikaribie ZINAA, hakika ya
hiyo zinaa ni uchafu na njia mbaya”
Hapo Mwenyezi Mungu amekataza
Zinaa, tena amesema hiyo zinaa ni
uchafu. Haya ni maneno aliyosema
Mwenyezi katika karne ya saba (7). Je?
Watu wa kanuni za maumbile
wanakubaliana kwamba ndani ya zinaa
kuna uchafu? Na kama upo ni upi?
Hatuwezi kuujua uchafu wa zinaa
mpaka tutazame katika mafundisho ya
wanasayansi wa sasa yaani MODERN
SCIENTISTS ili tujue wamekubaliana vipi
na Qur’an bila wenyewe kujua. Wakati
tunatafuta kujua uchafu wa zinaa na
madhara yake kisayansi lazima kwanza
tujue vitu vikuu vine:
(1) Uchafu ni nini?
(2) Manii yanatoka wapi kwa
mwanaume.
(3) Manii yanatoka wapi kwa
mwanamke.
(4) Na ndani ya manii mna nini.
Tunapozungumzia uchafu kwa tafsiri ya
jumla ni kitu kilichowekwa mahala
pasipostahili. Mfano; kuchukua kiatu
chenye thamani ya laki moja
ukakanyaga matope kisha kiatu kile
ukakiweka juu ya kitanda cha kawaida
na godoro la sufi ambacho thamani
yake kwa ujumla havifiki elfu arobaini;
lakini pamoja na thamani ya kiatu kuwa
kubwa kuliko kitanda na godoro mtu
akija atauliza huu uchafu aliyeweka
hapa juu ya kitanda ni nani? Kwa nini
aite kiatu cha gharama uchafu? Ni
kwamba kimekaa pahala pasipostahili.
Hivyo kitendo cha mwanaume au
mwanamke kupokea au kupeleka manii
yake pahala pasipokuwa halali yake huo
ni uchafu.
Kwa upande wa mwanaume
tunapozungumzia utoaji wake wa manii
ni mfinyo wa glands(tezi) za aina tano;
ambao mfinyo huu unapatikana baada
ya mwanaume kupata stimulation(msi
simko) na hapo ndipo tezi hizi hujibinya
na kutoa maji ya aina tano tofauti
yanayokutana katika makende na
kuchukua mbegu kisha yanatoka katika
hali na rangi ambayo wengi
tunaifahamu. Glands hizi za
mwanaume zimefungwa baina ya kifua
na mgogo.
Kwa mwanamke manii yake yanatoka
katika Glands za aina mbili tu ambazo
hizi zimefungwa katika kifua chake.
Hivyo maji haya yanayotoka katika
glands hizi mbili yakichanganyika na ya
mwanaume jumla yanakuwa maji ya
aina saba (7) yakikaa katika pahala
panapokusudiwa kwa mwanamke na
kwa muda maalum hapo ndipo
inapopatikana mimba na kizazi cha
binadamu kinaendelea.
Baada ya kujua hatua ya mwanzo
yanapotokea manii sasa tuingie katika
hatua ya pili ya kujua je? Ndani ya
manii mna kitu gani kitaalamu. Ndani
ya manii mna vitu vikuu vine:
• PROTEIN
• ACID
• SPERM/CHROMOSOME
• VIRUS
PROTEIN: Ni aina mojawapo ya “Food
Substance” inayorutubisha mwili.
Substance hii inapatikana ndani ya
manii na pia watu wa mambo ya
reproduction system (mfumo wa uzazi)
wanakubali kwamba manii yanatokana
na aina hii ya chakula na ndiyo maana
kama una njaa shughuli ya Jimai
inashindikana, au kama utajilazimisha
utapata madhara.
ACID: Ni mfano wa tindikali, yaani kitu
chenye ladha ya ukali mfano ndimu. Na
kitu chenye tindikali kina kawaida ya
kuunguza na pia kulegeza kwa
itakayompata au kumuingia, ndiyo
sababu kitaalam ukimlinganisha
mwanamke aliyeolewa na asiyeolewa
kisha akawa hafanyi zinaa maumbile
yao yanatofautiana. Yule aliyeolewa
mwili wake unakuwa laini zaidi sababu
ya acid inayopatikana ndani ya manii.
Nitakupa mifano mingi iliyo hai ili akili
yako ikubali kwamba vyote
vinavyotajwa vinapatikana ndani ya
manii. Ukitaka kuthibitisha zaidi acid ya
katika manii ambayo inaunguza
nakulegeza hata ukiwa na kidonda
kibichi ukitia manii kitauma mara mbili
zaidi sababu ya acid. Mfano mwingine
tazama kwa wale watoto wa kiume
ambao wanaingiliwa kinyume na
maumbile (mashoga) hata kama zamani
alikuwa strong (imara) kiasi gani
akiingiliwa tu, basi analegea kuanzia
kutembea, kuzungumza na kila kitu
sababu ni Acid inayopatikana ndani ya
manii. Pia ndio maana inakatazwa
kumuingilia mwanamke
anayenyonyesha sababu ukimuingilia
ukamuingizia manii ambayo yana acid,
acid ile itapanda katika maziwa na
kuyaharibu maziwa na hapo mtoto
akinyonya atanyonya maziwa yenye
acid. Itasababisha mtoto kulegea au
kwa watu wa pwani wanaita
kubemendwa, hivyo mtakua
mmemharibu mtoto. Lakini kama
atakula acid ya baba yake hatadhurika
sana, sababu atakula acid ambayo kwa
asili ndiyo iliyomtengeneza. Ila mkeo
akiziniwa na mtu mwingine mtoto
ataathirika sana na pengine itakuwa ni
sababu ya kifo chake kwa kuwa
amekula acid ambayo si ya asili kutoka
kwa wazazi wake hivyo itakuwa ni
POISON (sumu) kwake. Kazi kubwa ya
acid kwenye manii ni kuua bacteria
zisizohusika zinazopatikana wakati
zikitoka kuelekea katika virginal wall.
SPERM: Ni mbegu za kiume
zinazopatikana ndani ya manii na hizi
mbegu haziishi ndani ya mwili kwa
sababu ya hali ya joto la mwili, kwani
mtu wa kawaida ambaye haumwi
anakuwa na nyuzi joto 37 hivyo mbegu
zitakufa kutokana na joto la ziada.
Wataalamu wa mambo ya reproduction
na gynecology wanatueleza kwamba
mshindo mmoja una wastani wa watoto
milioni 200 hadi 300. Lakini
yanayofanikiwa kulifikia yai ni mia moja
tu. Na yanayofanikiwa kuingia kwa
kawaida ni moja au mawili yakizidi sana
manne tu, na si zaidi ya hapo, lau kama
yakizidi basi ni kwa miujiza yake
Mwenyezi Mungu.
VIRUS: Hivi ni vijidudu ambavyo kila
mtu anavyo vya kwake na pia
haviingiliani baina ya mtu na mtu na
hapa ndipo tutaeleza kwa kina madhara
ya zinaa kisayansi. Lazima pia tujue
kuwa Virus wanafanya kazi gani na pia
wanakwenda wapi. Katika virginal wall
kuna vijistomata (vitundu) maalum kwa
ajili ya kupokea virus; sababu
mwanaume anapotoa manii yake yenye
protein,acid,sperm/chromosomes na
virus kila kimoja huchukua nafasi yake
kwenda kunapohusika. Nafasi ya virus
ni kuingia katika vitundu vilivyo katika
virginal wall ili vipate kuishi humo kwa
kuwa ndipo alipowapangia Mwenyezi
Mungu. Hivyo basi ukiwa unamuingilia
mkeo na ukitoa manii basi moja kwa
moja virus wako watakwenda kuingia
katika vijitundu vilivyo kwenye virginal
wall ili kuishi humo. Ina maana virus
watakaoingia kuishi kwa mkeo ni wale
ambao wamezoeana. Sasa ikija kutokea
mkeo akazini na mwanaume mwingine
ataingiziwa virus wasiokuwa wako.
Hivyo hawa wapya wakiingia nao pia
watataka kuingia katika yale matundu ili
nao wakaishi. Kwa kuwa ndivyo
alivyowapangia Mwenyezi Mungu, hawa
wapya wakiingia tu wale wa zamani
ambao ni wa mume, watawashangaa,
watajiuliza hawa nao wametokea wapi?
Mbona si katika wale tuliozoeana? Kwa
kushangaa huku wale virus wenyeji
watawashambulia virus wageni kama
antibody bacteria (kitu kinachotoka nje
ya mwili). Na katika mapigano haya
watapelekea kundi moja kufa na kundi
moja likifa lazima wale waliokufa
watoke, watatoka vipi? Au watatokea
wapi? Jibu ni pale pale walipoingilia.
Hapo sasa ndipo mtu anapoanza
kutokwa uchafu. Na pia virus wapya
waliosalimika wakiona wanazidi
kushambuliwa na virus wa zamani
itabidi watoboe sehemu nyingine
zisizohusika ili wakimbie na kujificha
katika nyama laini.
Hapo ndipo mtu anapoanza kupata
maumivu makali wakati wa kukojoa na
pia ndio chanzo cha magonjwa
mbalimbali ya zinaa, na wakati huo
mume akimuingilia mkewe naye pia
atapata ugonjwa wa zinaa sababu
atakutana na virus wageni waliojificha
kujihami katika sehemu laini
zisizohusika watamuingia mume kupitia
mrija wa urinary truck (mrija wa
mkojo). Ndio sababu Mwenyezi Mungu
akasema zinaa ni uchafu. Na uchafu
unaokusudiwa ni kuchanganya mifumo
tofauti ya mwili yaani mwanamke
kuingiliwa na mwanaume zaidi ya
mumewe pekee. Na hapa ndipo
tunapoona hekima ya Mwenyezi
Mungu kwamba kwa nini ameamrisha
mwanamke kuolewa na mwanaume
mmoja na mwanaume kuoa
mwanamke zaidi ya mmoja. Hii ni kwa
sababu mwanamke anapokea manii
yenye kubeba VIRUS wa asili kutoka
kwa mumewe. Hapa ndipo
inapopatikana hekima ya ya
mwanamke aliyefiwa na mumewe au
aleyeachwa kwa talaka lazima akae
eda. Eda si tu kuangalia kama
mwanamke ana mimba, bali pia katika
kipindi cha miezi mine na siku kumi
ambacho mwanamke anakaa eda kwa
kuwa katika kipindi hicho haingiliwi ina
maana wale virus watakosa protein
inayopatikana katika manii ambayo ndio
chakula chao, hivyo kwa kukosa chakula
watakufa. Kwa hiyo katika kipindi hicho
mwanamke anaandaliwa ili kama
ataolewa tena na mume mwingine
huyu mume mpya ajitengenezee
mifumo yake mipya ambayo
haitapingana na ile ya mwanzo. Hivyo
Mwenyezi Mungu alipokataza ZINAA
anajua kwa kina madhara yake.
Ndio sababu twasema kwamba sera
bora za kupambana na magonjwa
mbalimbali ya zinaa kama UKIMWI n.k
dunia nzima ni kufuata UISLAM tu
hakuna la zaidi. Hivyo tunapenda watu
walifahamu hilo na kulifanyia kazi kwa
kuwa UISLAM siyo ugaidi wala si dini ya
vurugu bali ni dini ya AMANI ambayo
inaweza kumfaa mtu kimwili na kiroho.
Tunatoa wito kwa watu ulimwenguni
kote kumuamini Mwenyezi Mungu wa
kweli na Mtume wake wa karne ya
sayansi na teknolojia Nabii Muhammad
(S.A.W) ili kupata nusra ya mitihani
mizito na majanga yanayotukumba
wanadamu hivi sasa.

www.pilingu.blogspot.com

FAIDA ZA KIAFYA ZITOKANAZO NA ULAJI WA TENDE.

FAIDA ZA KIAFYA ZITOKANAZO KWA ULAJI WA TENDE. Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, tende ndiyo tunda linaloliwa kwa wingi, pengine kuliko tunda lingine. Pamoja na kuwa ni tunda lenye ladha tamu na nzuri mdomoni, lakini kisayansi pia limethibitika kusheheni madini na vitamini lukuki, hivyo kuwa na faida nyingi kiafya. Nimefanikiwa kukusanyieni faida kumi za tende mwilini nazo ni; 1. Ukila tende mara kwa mara, mwili wako utapata aina mbalimbali za madini na vitamin za kutosha, ambazo zinapatikana kwenye tunda hili maarufu duniani. Katika tende kuna kiasi kidogo tu cha mafuta (fat) na haina lehemu (kolestrol). 2. Ukila tende, utajipatia kiasi cha kutosha cha protini na vitamin B1, B2, B3, B5, A1, na C, virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ustawi wa afya ya mwili wako kwa ujumla. 3. Ulaji wa tende huimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji chakula tumboni, hivyo utaondokana na matatizo ya ukosefu wa choo, au matatizo ya kupata choo kigumu kinachosababisha maumivu wakati wa kujisaidia. Pia ndani ya tende kuna virutubisho vya ‘amino acids’ ambavyo ni muhimu mwilini. 4. Ukila tende, mwili utapata nguvu na kukuondolea uchovu ndani ya nusu saa tu, kwa sababu tende ina virutubisho vya sukari asilia kama vile ‘glucose’, ‘sucrose’ na ‘fructose’. Ili kupata faida zaidi za tende, changanya na maziwa fresh kisha kula. Unapojisikia mchovu, badala ya kunywa vinywaji baridi vinavyodai kuongeza nguvu, kula tende, hata kiasi cha punje tatu kinatosha. Kwa wafunga saumu, ndiyo maana inashauriwa kuanza kufungua kwa kula tende ili kuurejeshea mwili wako nguvu iliyopotea siku nzima. 5. Tende ina madini pia aina ya ‘potassium’ na kiasi kidogo cha chumvi (sodium). Madini haya husaidia uimarishaji wa mishipa ya fahamu. Watafiti wamegundua kwamba ulaji kiasi wa ‘potassium’ huweza kumuepusha mtu na kupatwa na kiharusi (stroke). Pia tende husaidia kupunguza lehemu (cholesterol) mwilini (LDL Cholesterol). 6. Kwa wale wenye matatizo ya ugonjwa wa kukauka damu mwilini (anemia), wanaweza kupata ahueni kwa kula tende kwa wingi ambayo ina kiwango cha kutosha cha madini ya chuma ambayo huhitajika katika utengenezaji wa damu mwilini. Wakati vitu vitamu vingine huozesha meno, utamu wa tende huzuia uozaji wa meno. 7. Kwa tatizo sugu na la muda mrefu la ukosefu wa choo, loweka tende za kutosha kwenye maji kiasi cha lita moja usiku kucha, kisha asubuhi changanya maji hayo pamoja na hizo tende ili upate juisi nzito, kunywa na choo kitafunguka na kuwa laini. 8. Kwa matatizo ya ukosefu wa nguvu za kiume, mchanganyiko maalum wa tende, maziwa, asali na unga wa hiriki vinaweza kuondoa tatizo lako. Chukua kiasi cha kiganja kimoja cha tende, loweka kwenye maziwa ya mbuzi kiasi cha lita moja na yakae usiku kucha. Asubuhi, zisage tende hizo kwenye maziwa hayo hadi zichangayike, kisha weka asali kiasi cha vijiko vitatu au vinne vikubwa pamoja na unga wa hiriki, kiasi cha nusu kijiko kidogo. Kisha kunywa mchangayiko huo kila siku hadi utakapoona mabadiliko ya kuridhisha. 9. Tende ni dawa ya unene, kwa wale wenye matatizo ya wembamba wa kupindukia na wanataka kuongeza uzito, ulaji wa tende kila siku unaweza kuwasaidia. Lakini hii ina maana kwamba, wale wanaohitaji kupunguza uzito, ulaji wa tende kwa wingi hauwezi kuwafaa. Pia tende husaidia uondoaji wa kilevi mwilini. 10. Tende inatibu saratani ya tumbo. Habari njema kuhusu tende kama tiba ni kwamba, haina madhara yoyote kwa sababu ni dawa asilia na inafanyakazi vizuri kuliko dawa za ‘kizungu’. Tende vile vile ina imarisha nuru ya macho na tatizo la kutokuona usiku (night blindness).