HEKIMA YA KULETWA MITUME.

MwenyeziMungu anasema:- "Bila shaka tumempeleka Mtume katika kila umma (awaambie) ya kwamba "Mwabuduni MwenyeziMungu na muepukeni (Iblis) muovu". (An - Nahl -36)

MAISHA YA BARZAKH (BAADA YA KUFA)

MwenyeziMungu anasema: "Hapana! Hakika hili ni neno tu analolisema yeye (aliye mwovu anapofikiwa na mauti) na mbele yao kuna maisha ya baada ya kufa (ya taabu kwa wabaya na ya raha kwa wazuri) mpaka siku watakapofufuliwa!". (Al - Muminun - 100)

VITISHO VYA SIKU YA KIAMA

Na katika kauli Yake:- "(Wakumbusheni) Litakapotokea tokeo (hilo la Kiama). Ambalo kutokea kwake si uwongo. Lifedheheshalo (wabaya). Litukuzalo (wazuri). Ardhi itakapotetemeshwa mtetemeko mkubwa. Na milima itakaposagwa sagwa. Iwe mavumbi yanayopeperushwa". (Al - Waqiah - 1 - 6)

KUMTII MWENYEZIMUNGU NA KUMTII MTUME WAKE(SAW)

MwenyeziMungu anasema:- "Na wenye kumtii MwenyeziMungu na Mtume, basi hao watakuwa pamoja na wale aliowaneemesha MwenyeziMungu; Manabii na Masidiki na Mashahidi na Masalih (watu wema). Na uzuri ulioje (kwa mtu) watu hao kuwa rafiki (zake).” (An - Nisaa -69)

KUTOKA KATIKA DINI -"KUR-TADI"

MwenyeziMungu anasema:- "Wala hawataacha kupigana nanyi, mpaka wakutoeni katika dini yenu, kama wakiweza. Na watakaotoka dini yao katika nyinyi, kisha wakafa hali ya kuwa makafiri, basi hao ndio ambao amali zao zimeharibika katika dunia na akhera. Nao ndio watu wa Motoni. Humo watakaa milele." (Al - Baqarah -217).

YAJUWE MAMBO 10 YANAYOHARIBU FIGO.

Kwa kifupi sana leo tunakutajia baadhi ya Tabia zinazochangia kuharibika kwa Figo. Tutambue kuwa tatizo hili la kufeli kwa figo limeshawakumba wengi na baadhi yao wameshapoteza maisha.
Ukiwa mzima mshukuru Mungu na ni vyema ukasoma makala hii ili kujinusuru na janga hili la kuharibikiwa figo.
Hizi hapa ni baadhi ya tabia 10 zinazoharibu figo:
1. Kubana mkojo kwa muda mrefu
2. Kutokunywa maji ya kutosha
3. Kutumia chumvi nyingi
4. Kula nyama mara nyingi zaidi
5. Kutokula chakula cha kutosha
6. Kuchelewa kujitibu maambukizi madogomadogo
7. Kutumia visivyo dawa za maumivu
8. Utumiaji wa madawa kwa ajili ya Insulin
9. Kunywa pombe kupita kiasi
10. Kutopata muda wa kutosha kupumzika

Ukiwa na tatizo la Figo njoo upate tiba sahihi na ushauri kituoni kwetu Sheikh Pilingu Ruqya &  Hijama Center
Au piga simu 0713494945
Email: pilingurashidi@gmail.com