HEKIMA YA KULETWA MITUME.

MwenyeziMungu anasema:- "Bila shaka tumempeleka Mtume katika kila umma (awaambie) ya kwamba "Mwabuduni MwenyeziMungu na muepukeni (Iblis) muovu". (An - Nahl -36)

MAISHA YA BARZAKH (BAADA YA KUFA)

MwenyeziMungu anasema: "Hapana! Hakika hili ni neno tu analolisema yeye (aliye mwovu anapofikiwa na mauti) na mbele yao kuna maisha ya baada ya kufa (ya taabu kwa wabaya na ya raha kwa wazuri) mpaka siku watakapofufuliwa!". (Al - Muminun - 100)

VITISHO VYA SIKU YA KIAMA

Na katika kauli Yake:- "(Wakumbusheni) Litakapotokea tokeo (hilo la Kiama). Ambalo kutokea kwake si uwongo. Lifedheheshalo (wabaya). Litukuzalo (wazuri). Ardhi itakapotetemeshwa mtetemeko mkubwa. Na milima itakaposagwa sagwa. Iwe mavumbi yanayopeperushwa". (Al - Waqiah - 1 - 6)

KUMTII MWENYEZIMUNGU NA KUMTII MTUME WAKE(SAW)

MwenyeziMungu anasema:- "Na wenye kumtii MwenyeziMungu na Mtume, basi hao watakuwa pamoja na wale aliowaneemesha MwenyeziMungu; Manabii na Masidiki na Mashahidi na Masalih (watu wema). Na uzuri ulioje (kwa mtu) watu hao kuwa rafiki (zake).” (An - Nisaa -69)

KUTOKA KATIKA DINI -"KUR-TADI"

MwenyeziMungu anasema:- "Wala hawataacha kupigana nanyi, mpaka wakutoeni katika dini yenu, kama wakiweza. Na watakaotoka dini yao katika nyinyi, kisha wakafa hali ya kuwa makafiri, basi hao ndio ambao amali zao zimeharibika katika dunia na akhera. Nao ndio watu wa Motoni. Humo watakaa milele." (Al - Baqarah -217).

Showing posts with label MATATIZO YA UCHAWI NA MAJINI. Show all posts
Showing posts with label MATATIZO YA UCHAWI NA MAJINI. Show all posts

UCHAWI:1



NINI MAANA YA UCHAWI?

Al Azhari ambaye ni
mtungaji wa kamusi
maarafu ya kiarabu iitwayo
“LisanulArab” amesema:
“Neno “Uchawi”, kwa
kiarabu “As Sihr”, maana
yake ni kitendo cha
kujikurubisha na shetani na
kwa msaada wake
(shetani)”, na akasema pia
kuwa; “Uchawi ni
kulibadilisha jambo mbali na
uhakika wake, nako ni
kuwadhihirishia watu jambo
lisilo la kweli wakaliona
kuwa ni la kweli.”
Ama Sahaba Ibni Abbas
(Radhiya Llaahu ‘anhu)
amesema:
"Uchawi ni kuidhirisha batili
katika sura ya haki."
Hayo ni katika kamusi za
lugha.
Amma katika kamusi ya dini,
maana ya neno Uchawi (As
Sihr), kama alivyofasiri
Mwanachuoni mkubwa
Fakhruddin Al Razi kuwa;
"Ni kila jambo lililofichika
sababu zake, linalotokeza
kwa sababu zisizo za
kawaida na ndani yake mna
hadaa (khidaa)."
Amma Sheikh Wahiyd
Abdulsalaam Bali, mwandishi
wa kitabu maarufu
kiitwacho 'Al Saarim Al
Batar fiy muhaarabat Al
Saharatul ashraar', na
kitabu kiitwacho "Al wiqaya
mina l jinni wa shaytan",
ambaye pia ni mtaalamu
maarufu katika elimu ya
majini na mashetani na
uchawi na ambaye pia ni
katika maulamaa maarufu
wanaotoa majini kwa njia ya
kusoma Qur-aan, yeye
anasema:
"Uchawi ni makubaliano
baina ya mchawi na Jinni
akishurutishwa mchawi
kufanya mambo ya haramu
au ya shirki, na baada ya
kufanya hayo, Jinni
anashurutishwa kumsaidia
na kumtii mchawi huyo kwa
kila anachotaka."
Baadhi ya yale ambayo
mchawi anatakiwa na
shetani ayatende ili
ajikurubishe naye ni:
 Mchawi anatakiwa auvae
msahafu miguuni na
aingie nao chooni
 Aandike baadhi ya aya
za Qur-aan kwa damu
ya hedhi.
 Miongoni mwao
wanashurutishwa
kuandika aya za Qur-aan
penye nyayo za miguu.
 Au aiandike suratulFatiha
kinyume nyume.
 Asali bila ya Udhuu.
 Wengine hutakiwa
kuchinja mnyama bila ya
kulitaja jina la
MwenyeziMungu kisha
amtupe mnyama huyo
mahali maalum
anapoamrishwa na
shetani.
 Wamo miongoni mwao
wanaozungumza na
nyota au kuzisujudia.
 Au hutakiwa kuandika
herizi kwa maneno yenye
kufru ndani yake
Imeelezwa kwamba katika
nchi ya Sham kulikuwa na
mtu ambaye watu walikuwa
wakimpenda na kumheshimu
sana wakimdhania kuwa ni
mtu mwenye makarama.
Mtu huyu alikuwa kila
mwaka katika msimu wa
Hajji akiwatumikia watu wa
mji wake kwa kuchukua
barua zao na vitu vyao na
kuwapelekea watu wao
waliokwenda Saudia kuhijji.
www.pilingu.blogspot.com
Alikuwa akipeleka na kurudi
kwa muda wa siku moja au
mbili tu, na watu
walimpenda sana na kuamini
kwamba alikuwa ni Waliy.
Siku moja mtu huyo aliumwa
sana, akamuita mwanawe
na kumwambia kuwa kama
atakufa, basi ende mahali
fulani wakati wa usiku na
atamkuta ngamia wa aina
fulani na ampande na
kufuata amri zote
atakazopewa na ngamia
huyo.
Alipofariki dunia, mwanawe
alifanya kama alivyoambiwa
na baba yake, akaondoka
peke yake wakati wa usiku
na kuelekea jangwani kule
alikoambiwa na baba yake
kuwa atamkuta ngamia.
Akamkuta ngamia kama
alivyoambiwa, akampanda
na alipokuwa akenda,
ngamia akaanza kusema na
kumtaka kijana yule ashuke
na amsujudie.
Yule kijana alistuka sana
kusikia ngamia akisema na
pia akashangazwa na amri
zake, akamwambia:
"Vipi nikusujudie, kweni
wewe ni nani?"
"Ikiwa unataka nifuate amri
zako kama nilivyokuwa kwa
baba yako, na nikupeleke
popote utakapo duniani, basi
unisujudie kama alivyokuwa
akinisujudia baba yako."
Yule kijana akajibu:
"Mimi ninamsujudia
Mwenyezi Mungu peke yake,
amma wewe la, siwezi
kukusujudia."
Ngamia akamrusha kijana
yule kutoka juu ya mgongo
wake na kumwangusha
chini, na kijana yule akatoka
mbio mpaka nyumbani kwa
mama yake na kumuelezea
yote aliyoyaona na kwamba
baba yake alikuwa
akimsujudia Jinni ndiyo
maana alikuwa na uwezo
wa kusafiri kila anapotaka
kwenda kwa kupaishwa na
jini yule.
Kwa haya inatubainikia
kuwa Jinni hamsaidii wala
hamhudumii mchawi wala
mtu yeyote isipokuwa naye
kwa mkabala wake
atumikiwe kwa kutendewa
matendo ya kufru, na
maulamaa wanasema:
"Kila mchawi anapokufuru
zaidi, basi shetani
humtumikia kwa nguvu
zaidi, na mchawi akitaka
apate huduma ya hali ya juu
kabisa kutoka kwa
masultani wa majini au kwa
kiarabu wanaitwa
"Maradatul Jinni", basi
inambidi afanye kufuru
kubwa zaidi, na kwa ajili
hiyo, mchawi anapotaka
nguvu juu ya wenzake
inamlazimikia akufuru zaidi."
Kutokana na haya
tunafahamu kwamba
mchawi na shetani ni
marafiki na washirika katika
kumuasi MwenyeziMungu.
MwenyeziMungu Anasema:
"Na (wakumbushe) siku
atakapowakusanya wote
(akawaambia): "Enyi
makundi ya majini! Hakika
nyinyi mmechukua wafuasi
wengi katika wanaadamu".
Na marafiki wao katika
wanaadamu
(watagombania) waseme:
"Mola wetu! Tulinufaishana
sisi na wao na tumefikia
muda wetu uliotuwekea".
Basi (Mungu) atasema;
"Moto ndio makazi yenu,
mtakaa humo milele", ila
apende MwenyeziMungu
(kuwarehemu), hakika Mola
wako ndiye Mwenye hikima
(na) ndiye ajuaye.”
Al An - Am - 128
Je, Utamjuaje mchawi???
Usipitwe na sehemu ya 2.

UTAMJUAJE MTU ALIYEATHIRIKA NA UCHAWI AU MAJINI?.


1.  Kuumwa kichwa upande mmoja,meno,mgongo,kiuno na kubanwa kifua.
2.  Kuumwa tumbo chini ya kitovu hii ni kwa akinamama.
3.  Moyo kwenda mbio na kushtuka bila asbabu.
4.  Kushika moto mwili hasa miguu pmj na ganzi na maumivu makali.
5.  Kizunguzungu mara kwa mara.
6.  Kuumwa tumbo sana kwa akinamama wakati wa period pmj na kutoa damu nyingi au chache sana.
7.  Kupata maumivu makali wakati wa jimai kwa akinamama na kukosa hamu ya tendo hilo au kulichukia kabithaaaa.
8.  Kutembelewa na vitu mwilini.
9.  Kutingishika,kutetemeka sana na kulia bila sababu ikiwemo na hasira sana.
10.  Kuhisi uzito wa mwili kana kwamba umebeba mzigo mzito.
11.  Chuki ndani ya ndoa kutamani kuachwa au kuacha bila asbabu.
12.  Maneno machafu kwa mwenza na punde tyuu majuto mjukuu.
13.  Kufungika hedhi bila sababu na kutoshika ujauzito bila sababu za msingi.
14.  Kuota umjauzito,unazaa,unanyonyesha na unabeba watoto.
15.  Kujaa kitumbo ndiiii bila ujauzito na kuchezacheza kitu tumboni bila ya ujauzito.
16.  Kuharibika mimba baada ya kuota unafanya vituuuuz na mtu atishae au hata umjuae au usiyomjua.
17.  Kuyeyuka na kuharibika mimba bila sababu za msingi.
18.  Ndoto za jimai mara kwa mara.
19.  Kuwa na hamu sana ya mambo yetu yaleeeeeee uwapo peke yako lkn ukutanapo na mwenza hamu hiyooooo ishasepa na kwa mume hupotelewa na nguvu ghafla.
20.  Kuvurugika mipango ya kuoa au kuolewa mara kwa mara.
21.  Kuhisi unaingiliwa au kuingilia babaweeeee hii sio ndotonivyoooooo uvitambue babaaaaaa.
22.  Kutopenda ibadah lkn maasi unayapa mahabba mazitooo.
23.  Hasira,uvivu pmj na hofu bila sababu.
24.  Kuhisi kusimamiwa na mtu mbele yako,nyuma,pembeni na hata ulalapo na kuwa na hofu sana juu ya hilo.
25.  Kukosa usingizi au usingizi mzito mpk swalat subhi ikakupita.
26.  Usomapo Qur-an au kusikiliza hotuba ya ijumaa hupata usingizi a.k.a kusinziasinzia lkn usomapo magazeti au mazungumzo mengine usingizi hauji ng'oooo.
27.  Tamaa kupita kiasi na kujihisi ni mtu wa thamani sana kinyume na ulivyo.
28.  M/mke kupenda kujiremba awapo nje ya nyumba yake lkn akiwa ndani kwake huwa hajirembi na km ana mume basi hubaki kumuachia harufu mbaya mumewe. loh wanawake nyiyeeee loh hebu jirembeni mkiwa ndani ili sisi waume zenu tujihisi kupendwa nasi tukazidisha upendo.
29.  Kupenda vitu vya upuuzi km vile miziki,porojo,udaku,vipindi vya TV visivyo na maana au redio.
30.  Kuota ndoto za vitisho km vile wanyama wakali,au unafanyiwa uadui au unazingirwa na maji,kifo,jeneza,unatumbukia shimoni na unapaa hewani wala mbawa hauna.
31.  Kuota ibada zisizo na mwelekeo.
32.  Kulia,kucheka na kupiga kelele usingizini a.k.a Jinamizi.
33.  Kuchanganyikiwa ndani ya swala pmj na kuyumba na kusinzia usiisahauvyooo.
34.  Kuota mtu mfu au unaelezwa jambo ndotoni na ikiwa yote ni kweli hali hauna Uchamungu na hivyo.
35.  Kuota watu watishao.
36.  Kuota sana nyumba za ibada (misikiti)hali wewe si mtu wa ibada.
37.  Kuota unafanya mashauri na watuwafu a.k.a Mizimuuu.
38.  Kuota unafanyiwa shughuli zote za mazishi au unamfanyia mwenzio.
39.  Kuota unaingiliwa au unaingilia kinyume na maumbile a.k.a Liwatwi.
40.  Kushtukashtuka mara kwa mara usingizini.
41.  Kuibiwa pesa hata uzifungie waaaaapi vileeeee a.k.a Chumaulete.
Haya ndg zangu hizo ndio dalili 41 nilizosema nitawaekea na zipo nyingi zote hizo zinaashiria mtu kusumbuliwa na shetani wa kijini (wachawi) na mtu sio lzm awe nazo zote